Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wizara zimeagizwa kufanya kazi kwa karibu na wakulima wa mwani.
WIZARA ya Biashara Viwanda na Masoko, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto zimeagizwa kufanya kazi kwa karibu na wakulima wa mwani ili kuhakikisha kuwa bei wanayolipwa wakulima hao inalingana na nguvu na gharama wanazozitumia sambamba na hali halisi ya bei ya bidhaa hiyo katika soko la nje.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa agizo hilo leo huko ukumbi wa Salama, katika Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar mara baada ya kukabidhi vihori vya kubebea mwani kwa wakulima wa mwani wa Unguja na Pemba . Katika hotuba yake Dk. Shein alisema kuwa ni wajibu wa Serikali kuwaunga mkono wananchi kwa kuwajengea uwezo, ikiwemo kuwapatia masoko, mafunzo muhimu na fursa za mikopo pamoja na kuongeza kasi katika kutafuta masoko mapya. Dk. Shein alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kutaka kuona kuona kuwa wakulima wa zao la mwani wanaongeza kiwango cha uzalishaji wa mwani na uwezo wao wa ubunifu katika kutumia rasilimali zilizoizunguka Zanzibar, ili waweze kujikwamua kiuchumi na kufikia malengo la Mpango wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana na Umasikini Zanzibar awamu ya pili (MKUZA II). Aidha, Dk. Shein alieleza haja ya kufanywa utaalamu uliotumika hadi bei ya karafuu ikaongezeka kufanywa pia, kwa upande wa bei ya zao la mwani huku akieleza kuwa Serikali itaendeleza jitrihada zake za kuwanga mkono wakulima wa mazao mbali mbali na kuhakikisha kuwa bei wanazolipwa kwa mazao yao inalingana na jitihada zao. Dk. Shein alihimiza kuwepo kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) kwa ajili ya kufanya utafiti juu ya njia bora za kuzalisha zao hilo ikiwa nji pamoja na kuwatafutia wakulima mbegu bora. Pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa nasaha zake kwa wale wote waliobahatika kupewa vihori hivyo kuvifanyia kazi ipasavyo na kuvitunza huku akiahidi Serikali kuendelea kutafuta njia zaidi za kuwasaidia wakulima wa mwani hapa nchini. “ Vihori hivi vya kisasa vitawapa nafuu wakulima wa mwani, hasa wanawake.. nafahamu jitihada za kina mama katika uzalishjaji wa zao hili..matarajio yangu ni kuwa vihori hivi vitasaidia kuondoa tatizo la ubebaji na vitatoa msukumo katika kuongeza kiwango cha uzalishaji na hatimae muongeza kipato cha wakulima’,alisema Dk. Shein. Kwa upande wa utunzaji wa mazingira, Dk. Shein aliwataka wakulima wa mwani kukumbuka kuwa wakidharau umuhimu wa kuyatunza mazingira wataweza kuathiri shughuli za uvuvi na hata za utalii na kusisitiza kuwa kuweka safi mazingira ni jambo muhimu sana. Sambamba na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza azma ya serikali katika kuimarisha sekta ya uvuvi ambayo hapo siku za nyuma ilikuwa na mafanikio makubwa na hivi karibuni kukabiliwa na changamoto na kusisitiza kuwa Serikali imeandaa Sera ya Mkifugo na Uvuvi, ina mpango wa kuanzisha Kampuni ya uvuvi, kununua boti za maaluma na za kisasa za uvuvi na kuanzisha kiwanda cha kusindika samaki hapa nchini. Alisema kuwa tayari Serikali imeshafanya mazungumzo na mwekezaji kutoka nje kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi kwa kuanzia na rasilimali ziliopo nchini. Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali itasimamia ipasavyo mambo yote ya msingi katika masuala yua uwezeshaji, ili kuona wakulima wa zao la mwani na mazao mengine wanakua na kuondokana na changamoto zinazowakabili na kukuza kipato chao. Kabla ya hotuba yake Dk. Shein alikabidhi vihori hivyo kwa vikundi vya Unguja na Pemba kwa niaba ambapo mapema katika vuiwanja vya ukumbi huo alikagua maonyesho maalum yaliohusisha bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa kwa kutumia mwani zikiwemo mafuta, sabubi za kukogea na kufulia pamoja na vyakula mbali mbali vinavyopikwa kwa kutumia mwani na mazao mengine ya bahari. Nae Waziri wa Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohammed, alieleza mikakati iliyowekwa na Wizara yake katika kuhakikisha zao hilo linapata mafanikio Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Bi Asha Ali Abdalla alisema kuwa moja ya majukumu ya Wizara ni kusaidia uanzishwaji wa makongano ya biashara, kama miongoni mwa mikakati ya kuwawezesha wananchi kiuchumi. Alisema kuwa wazo la upatikanaji wa vihori hivyo linatokana na utafiti mdogo uliofanywa na mfanyakazi wa kujitolea kutoka Shirika la Kimataifa la Huduma za Kujitlea Bwana Hossein Chehrzade kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Idara ya Uratibu na Uendeshaji wa Programu za Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi, pamoja na Dk. Flower Msuya wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Tanzania. Katibu Asha alisema kuwa jumla ya vihori 100 vimenunuliwa kwa kuazia na vitagawiwa Unguja na Pemba kwa uwiano wa 30 kwa Unguja na 70 kwa Pemba ambapo jumla ya vikundi vidogo vidogo 63 vya wakulima wa mwani na wakulima mmoja mmoja 14 watanufaika na vihori hivyo. Aidha, alisema kuwa wanufaikaji wote wa mradi huo ni 448, kati ya hao 313 ni kutoka Pemba na 135 Unguja, wakiwemo wanawake 364 na wanaume 84 na kusisitiza kuwa vihori hivyo vina uwezo wa kubeba kilo mia nne za mwani mbichi kwa mara moja. Alisema kuwa kwa kutumia vihori hivi, uwezo wa wakulima wa kubeba mwani kupeleka ufukweni utaongezeka kutoka kilo 50 hadi kilo 400, sawa na ongezeko la asilimia 87.5, ongezeko ambalo linatarajiwa kuongeza uzalishaji wa mwani hapa Zanzibar sambamba na kuongeza kipato kwa wakulima wa zao hilo. Nao wakulima wa zao la mwani katika risala yao walieleza kuwa kutokana na upatikanaji wa vihori hivyo wataweza kuongeza uzalishaji, kuokoa mwani mwingi ambao hubururwa na maji na kukuza soko la mwani hapa Zanzibar. Wakulima hao wa mwani waliiomba Serikali kufanya kila liwezekanalo kuwapatia mambo yote ya msingi yatakayopelekea kuimarika na kudumu kwa shughuli zao za mwani ikiwemo kupandishiwa bei kwa zao hilo. Sambamba na hayo waliahidi kuvitunza vihori hivyo na kufuata masharti yote ambayo wamepewa ili vihori hivyo viweze kudumu kwa muda mrefu na kuongeza uzalishaji wa mwani hapa nchini. Nao Wawakilishi kutoka COSTECH pamoja na kutoka Shirika la Kimataifa la Huduma za Kujitolea VSO, waliahidi kuendelea kuwaunga mkono wakulima wa zao hilo mwani hapa Zanzibar ili liendelee kutoa ajira na kuongeza kipato cha wakulima na Taifa kwa jumla. Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali walihudhuria wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, viongozi wa Serikali na wananchi mbali mbali wakiwemo wakulima wa mwani kutoka Unguja na Pemba ambapo pia, shughuli hiyo ilipmbwa kwa ngoma ya Kibatim utenzi.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo