Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Dk.Shein atembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria uwanja wa ndege.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amefanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.Dk. Shein alifanya ziara hiyo mapema leo asubuhi akiwa ameongozana na viongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum, uongozi wa Wizara ya Fedha na viongozi wengineo wa Mamlaka ya Uwanja huo. Dk.Shein atembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria uwanja wa ndege. . Mapema Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk. Malick Akili ambaye alimueleza hatua zinazoendelea katika ujenzi wa jengo jipya la abiria pamoja na mradi wa ujenzi wa uzio katika uwanja huo.Katika maelezo yake, Dk. Malick alisema kuwa ujenzi wa jengo la abiria unaendelea vizuri hivi sasa chini ya Kampuni ya Kichina ya Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd (BCEG).Katibu Mkuu huyo alitoa maelezo juu marekebisho ya ujenzi wa jengo jipya la uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume pamoja na hatua za ujenzi wa uzio unaozunguka uwanja huo. Akieleza kuhusu mradi wa ujenzi wa uzio, Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hadi kufikia hivi sasa sehemu iliyowazi ambayo mkandarasi anaendelea na kazi ni takriban mita 500 iliopo sehemu ya Kaskazini Magharibi ya kiwanja na kusisitiza kuwa ili kukamilisha eneo hilo la uzio kwa kipande cha mita hizo jumla ya TZS milioni 560 zinahitajika.Aidha, Dk. Shein kabla ya kuanza ziara hiyo alitembelea kituo cha Zimamoto na Uokozi kiliopo uwanjani hapo na kupata maelezo juu ya uimarishaji wa Kikosi cha Zimamoto kiwanjani hapo kutoka kwa uongozi wa Kikosi hicho. Katika ziara yake kwenye ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na kutoka kwa Mshauri Elekezi mpya wa Kampuni ya ADPI ya Ufaransa bwana Verna Guillaume.Kwa mujibu wa maelezo ya Mshauri Elekezi wa Kampuni ya ADPI bwana Guillaume kutoka Ufaransa, alimueleza Dk. Shein hatua za ujenzi zinazoendelea vizuri huku akitoa maelezo juu ya marekebisho kadhaa ya ujenzi huo unaoendelea ambayo yatasaidia katika kufikia lengo lililokusudiwa. Nae, Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa jengo jipya la abiria Bwana Yasser De Costa alitoa maelezo kadhaa kwa Mhe. Rais juu ya ujenzi huo unaoendelea ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma kwa wageni na wenyeji wanaosafiri kupitia jengo hilo jipya na la kisasa.Ongezeko la eneo la jengo baada ya masawazisho hayo ya kiufundi yatapelekea kuongezeka kwa uwezo wa jengo hilo kuhudumia jumla ya abiria milioni 1.6 badala ya abiria milioni 1.1 iliyopangwa kupitia mkataba wa awali. Sambamba na hayo, takwimu zinaonesha kuwa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume kinakadiriwa kuchukua abiria wapatao milioni 2 ifikapo mwaka 2025, hatua ambayo pia, itachangia kukuza uchumi na kuimarisha sekta ya utalii hapa Zanzibar.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo