Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Zanzibar na Msumbiji kubadilishana uzoefu na Utalaamu katika Sekta mbalimbali za Maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema wakati umefika kwa Zanzibar na Msumbiji kubadilishana uzoefu na utalaamu katika sekta mbalimbali za maendeleo na uchumi ikiwa njia mojawapo ya kukuza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya serikali na wananchi wa pande mbili hizo.Akizungumza na Rais wa Msumbiji Bwana Filipe Jacinto Nyusi Ikulu leo, Dk. Shein alimueleza Rais huyo kuwa historia inaonesha kuwa uhusiano kati ya watu wa Zanzibar na Msumbuji umedumu kwa karne nyingi kabla ya uhuru hadi leo ambapo watu wa pande mbili hizo wamekuwa na uhusiano na ushirikiano wa karibu. Kwa hivyo alisema ni wakati muafaka kwa pande hizo kuangalia namna ambavyo zinaweza kutumia fursa zilizopo katika maeneo ya ushirikiano kuimarisha uhusiano kati yao na wananchi.Dk. Shein alitaja sekta ya utalii kuwa ni mojawapo ya maeneo Zanzibar na Msumbiji zinaweza kubadilishana uzoefu halikadhalika sekta ya uvuvi ambayo Zanzibar haijapiga hatua katika kuiendeleza sekta hiyo.Alimueleza Rais huyo kuwa eneo jingine la ushirikiania ni elimu na mafunzo kupitia ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar-ZUSA na vyuo vikuu vya Msumbiji. Aliongeza kuwa sekta ya biashara ni sekta muhimu ambayo pande hizo zilikuwa zikishirikiana kwa miaka mingi na kudokeza kuwa kufuatia Serikali ya Zanzibar kununua meli mpya safari za kibiashara kati ya bandari za nchi hizo zinaweza kuanzishwa tena. Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimpongeza Rais Nyusi kwa ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu uliopita nchini Msumbuji ambapo yeye akiwa mgombea kupitia chama cha FRELIMO alishinda ambapo alimueleza kuwa Tanzania imefurahishwa sana na ushindi wa chama cha FRELIMO kwa kuwa ushindi wa chama hicho ni ushindi wa watanzania wote.Alibanisha kuwa ziara ya Rais Nyusi nchini Tanzania ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo kati ya Msumbiji na Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa upande wake Rais wa Msumbiji Bwana Filipe Nyusi alisema ziara yake nchini Tanzania ina lengo la kudhihirisha dhamira ya Serikali na wananchi wa nchi yake kuimarisha uhusiano wake na Serikali na wananchi wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Alibainisha serikali na wananchi wa Msumbiji wanathamini sana uhusiano wao na serikali na wananchi wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Nyusi alieleza kuwa wananchi wengi wa Msumbiji wamekuwa wakiishi nchini Tanzania kwa furaha na mapenzi makubwa kutoka kwa ndugu zao wa Tanzania hivyo ni jambo la kujivunia sana kwao.Aidha, alisema Msumbiji na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa na kidiplomasia hivyo ni wakati sasa kupanua uhusiano huo katika mameneo mengine yakiwemo ya uchumi.Kwa hivyo alieleza kuwa nchi yake ingependa kuona kunakuwepo na ushirikiano mzuri katika sekta kama ya utalii ili kukuza biashara hiyo kati ya nchi yake na Zanzibar. Hivyo alibanisha kuwa ni wazo zuri kuangalia fursa zilizomo miongoni mwa nchi hizo kwa kuimarisha mawasiliano ya karibu ili kutimiza azma hiyo.Rais Nyusi alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na wananchi na viongozi wa Zanzibar kwa mapokezi makubwa aliyopewa alipowasili Zanzibar.Rais Nyusi aliwasili leo mchana akitokea Dar es salaam ambako alianza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Tanzania. Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo