Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Serikali itaendelea kutoa elimu bure kwa watoto
STATE HOUSE ZANZIBAR OFFICE OF THE PRESS SECRETARY PRESS RELEASE Zanzibar 14.6.2015 --- LICHA ya kupanda kwa gharama za uendeshaji wa sekta ya elimu hapa Zanzibar na duniani kote, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa bure kwa watoto wa Zanzibar kama ilivyotangazwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, tarehe 23 Septemba, 1964. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameyasema hayo leo huko katika viwanja vya skuli ya Ndijani iliyopo Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja katika kilele cha Sherehe za kutimiza miaka 90 tokea kuanzishwa kwa skuli hiyo. Katika hotuba yake iliyosema kwa niaba na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, Mhe. Ali Juma Shamuhuna, Dk. Shein alisema kuwa uamuzi alioufanya wa kuondoa uchangiaji wa fedha kwa wazazi katika skuli zote za Msingi za Zanzibar alioutangaza terehe 12, Januari, 2015 katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi, una lengo la kuendeleza dhamira hiyo. Dk. Shein alisema kuwa amefurahishwa kuona kuwa Wizara ya Elimu inalifanyia kazi agizo hilo na kuendelea kuwaelimisha walimu na wanafunzi na wazee juu ya madhumuni ya agizo hilo. Alisema kuwa agizo hilo tayari limeshaanza kutekelezwa, ambapo wanafunzi waliomaliza mitihani yao ya Kidato cha Sita hivi karibuni hawakulipa ada za mitihani na kuwataka kuongeza jitihada ili wafaulu vizuri mitihani yao. Aidha, aliwaeleza wazee kuwa wanawajibu wa kuendelea kuwa karibu na wanafunzi hao ili wawasaidie na kuweza kuwaelekeza njia bora za kuwajengea misingi imara kwa maisha yao ya baadae. Dk. Shein alisisistiza kuwa, njia bora ya kuzidi kuitunza historia ya Skuli hiyo ni kuhakikisha walimu, wazazi na wanafunzi wa zamani wa skuli hiyo wanaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kwa lengo la kuifanya kuwa ni chimbuko la kutoa watu maarufu na wataalamu katika nyanja zote wakiwemo viongozi, wanasanyansi, maprofesa, watafiti na nyota wa wanamichezo mbali mbali. Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kufurahishwa kutokana na skuli hiyo kufanya vizuri katika michezo mbali mbali, hasa mchezo wa riadha, kwani imeweza kutoa upinzani mkubwa kwa wanariadha wa Skuli ya Filbert Bai katika mashindano ya Mbio za Nyika, yanayofanyika kila mara hapa Zanzibar. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi wa Skuli ya Ndijani kwa kuandaa maadhimisho hayo ya miaka 90 kwa mtindo wa aina yake. Alisema kuwa uongozi wa Skuli hiyo pamoja na wananchi wa eneo hilo wameonesha mfano kwa vitendo juu ya umuhimu wa kuweka kumbukumbu na kuithamini historia ya vijiji, skuli, taasisi na nchi kwa jumla. “Mmeweza kuitunza historia ya skuli hii tokea siku ilipoanzishwa pamoja na kufuatilia maendleo ya watu waliosoma hapa, kazi mbali mbali walizofanya na nyadhifa muhimu walizoshiriki Serikalini, katika taasisi binafsi pamoja na Asasi za Kirai...Nimefurahi kwa uwekaji wenu mzuri wa kumbukumbu. hongereni sana”,alisema Dk. Shein. Sambamba na hayo, Dk. Shein alisema kuwa Sekta ya elimu kama zilivyo sekta nyengine ina historia kubwa ambayo inapaswa kusomwa na kuifahamu ili kuendelea kuyathamini mafanikio makubwa yaliopatika katika kipindi hiki cha miaka 51 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibae ya mwaka 1964. Dk. Shein alisema kuwa historia ya skuli ya Ndijani inalingana na historia ya skuli ya Dole iliyoanzishwa mwaka 1935 na kupewa jina la “Rural Middle School Dole” na Skuli ya Makunduchi ambayo ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, akuli ambazo ni za mwanzo zilizoanzishwa nje ya mji wa Unguja na kutoa fursa kwa wanyonge. Katika risala ya wazazi, walimu na wanafunzi iliyosomwa na Mwalimu Saleh Kasim, ilieleza kuwa skuli ya Ndijani ni miongoni mwa Skuli kongwe hapa Zanzibar iliyojengwa rasmi mwaka 1925. Risala hiyo ilieleza kuwa miongoni mwa viongozi waliosoma skulini hapo ni Mhe. Ali Khamis Spika wa Kwanza wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban, Mhe.Mtumwa Kheir Mbarouk, Mhe. Haji Makungu Mgongo, Mhe. Maulid Makame Juma Dk. Issa Haji Zidi, Marehemu Dheikh Mussa Makungu, marehemu Dk. Dalu na wengineo. Wananchi hao pia, aktika risala yao walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa kuiongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mafanikio makubwa, busara na hekima ya hali ya juu. Mapema Mhe. Shamuhuna alitembelea mabanda ya maonesho ambapo pia katika sherehe hizo kulifanyika mnada na harambee ya vitu mbali mbali pamoja na kutoa vyeti na zawadi kwa watunukiwa ambapo viongozi mbali mbali walihudhuria. Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo