Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wafanyabiashara wote nchini wametakiwa kutopandisha bei za bidhaa zao katika mwezi wa Ramadhani
Wafanyabiashara wote nchini wametakiwa kutopandisha bei za bidhaa zao katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani bila ya sababu za msingi na kuwafikiria wananchi hasa wanyonge kwani hatua hiyo ni kinyume na malengo ya Serikali ya kupunguza unafuu wa kodi kwa bidhaa za chakula.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo huko Ikulu mjini Zanzibar katika risala yake ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. Wafanyabiashara wote nchini wametakiwa kutopandisha bei za bidhaa zao katika mwezi wa Ramadhani Katika risala yake hiyo Alhaj Dk. Shein alisema kuwa wafanyabiashara wasivutiwe na kutaka kupata faida kubwa, bali wawafikirie wananchi wenzao kwani si jambo la busara kuutumia mwezi huu kwa kuwapandishia bei wananchi, hasa wanyonge.Alhaj Dk. Shein alisema kuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani shughuli za biashara huimarika zaidi hivyo aliwasihi wafanyabiashara kuendelea kuzingatia sheria na kusisitiza biashara zote zifanywe katika maeneo yalioruhusiwa ili kuepusha usumbufu na msongamano usio wa lazima. Aliwataka wafanyabiashara pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Manispaa kwa mji wa Unguja na Mabaraza ya Mji wa Pemba, kuongeza juhudi zao katika kuimarisha usafi wa miji kwani uzoefu unaonesha kuwa katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani taka huongezeka.Alieleza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na wafanyabiashara katika utekelezaji wa Sera ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutoa unafuu wa kodi katika uingizaji nchini bidhaa muhimu za chakula ikiwemo mchele, unga wa ngano, sukari na tende. Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa lengo la uamuzi huu wa Serikali ni kuhakikisha kuwa chakula cha kutosha kinakuwepo katika kipindi chote cha Mwezi wa Ramadhani na kinapatikana kwa bei nafuu zaidi.Akieleza kuhusu wakulima wenye tamaa ambao huamua kuleta sokoni mazao ambayo hayajapea, Alhaj Dk. Shein alizitaka taasisi zinazohusika kusimamia taratibu na utekelezaji wa Sheria ya kumlinda mtumiaji, ikiwa ni pamoja na kuwaepusha wananchi kuuziwa bidhaa ambazo muda wake wa matumizi umemalizika.“Tuna wajibu wa kujiandaa na kuweka azma ya kuzidisha Ibada kwa wingi ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yote ya Kheri, kusali sala za faradhi na sunna na kujifunza pamoja na kusoma sana Kurani”,alisema Alhaj Dk. Shein. Aidha, Alhaj Dk. Shein aliendelea kuiagiza Mamlaka ya Maji ya Zanzibar (ZAWA) na Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kufanya kila jitihada ili iwapatie maji wananchi kwa kutumia magari katika maeneo yote ambayo huduma hiyo ina upungufu.Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa katika mazingatio ya kufanya wema na kufuata maadili yanayotukuzwa katika mwezi wa Ramadhani, wananchi wanapaswa kuzingatia umuhimu wa kudumisha na kukuza amani na utulivu. Alisisitiza kuwa Ibada ya saumu inahitaji kuwepo kwa utulivu wa nafsi ili kuwapa watu kuitekeleza Ibada hiyo yenye malipo makubwa kwa MwenyeziMungu ambapo katika suala hilo watu wote wana wajibu wa kusimamia amani na utulivu ili utekelezaji wa ibada hiyo usiathirike.Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa katika kufunga yapo mambo ya kuharibu funga ya mfungaji ambapo miongoni mwa mambo hayo ni kusema uongo na kufitini watu, hivyo aliwataka wananchi kujiepusha na mambo ya aina hiyo na badala yake wazidishe mapenzi baina yao, wahurumiane na kusaidiana katika ambo ya kheri. Wakati huo huo, Alhaj Dk. Shein aliwasihi wenye kumiliki mikahawa washirikiane na waumini wanaotukuza Mwezi huo katika kuondoa kero ambazo zinaweza kuwasababishia karaha wanapoitekeleza Ibada ya funga.Aliwataka wananchi kuheshimu utamaduni walionao wa kuheshimu dini, jambo ambalo limechangia kudumu kwa amani ya nchi tangu kale na dahari na kusisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kuhakikisha kuwa Mwezi wa Ramadhani unaheshimiwa kwa vitendo. Pia, aliwataka wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao nyakati za usiku, ili wawe na nyendo njema pamoja na kuwashajiisha kufanya ibada na kudumisha darsa misikitini. Aidha, alivitaka vyombyo vya ulinzi kuimarisha doria za ulizni katika maeneo mbali mbali, hasa kwa wakati ambao watu wengine wanakuwa katika shughuli za Ibada.Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwakumbusha madereva kuzingatia sheria za usalama wa barabarani kwa kutoendesha gari na vyombo vyengine kwa mwendo wa kasi kwa kisingizio cha kutaka kuwahi kufutari sambamba na kupakia abiria zaidi jambo ambalo huhatarisha usalama wao. Sambamba na hayo, Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwatakia wananchi kheri, rehema na baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kumuomba MwenyeziMungu kuwapa wananchi uwezo wa kuendeleza Ibada za saumu na ibada nyengine katika mwezi huu pamoja na kudumisha na kuendeleza amani, umoja na mshikamano.Alhaj Dk. Shein, Alimuomba MwenyeziMungu kuwapa baraka wale wote wanaojiandaa na watakaojaaliwa kwenda kuhiji mwaka huu kuwajaalia kheri na safari ya salama.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo