Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Kenya na Tanzania ni nchi zenye uhusiano wa muda mrefu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Kenya na Tanzania ni nchi zenye uhusiano wa muda mrefu hivyo kuna kila sababu za kuendelea kuimarisha na kuitekeleza Sera ya Demokrasia ya Uchumi kwa manufaa ya pande mbili hizo.Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya Mhe. John Michael Haule, ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya kuaga na kupata baraka za Rais. Kenya na Tanzania ni nchi zenye uhusiano wa muda mrefu. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Haule kuwa kwa vile Kenya na Tanzania zimo katika mchakato wa kutekeleza Sera ya Demokrasia ya Uchumi ana matumani makubwa kuwa mafanikio makubwa ya kiuchumi yataendela kupatikana baina nchi mbili hizo.Dk. Shein alisema kuwa mashirikiano katika nyanja mbali mbali za maendeleo hasa ikizingatiwa nchi mbili hizo zimo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yamekuwa yakiimarika siku hadi siku. Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa nchi mbili hizo zimekuwa na historia ya kusaidiana pale nchi moja wapo inapopata matatizo, hivyo ana imani kubwa na Balozi Haule kuwa ataendeleza uhusiano na ushirikiano huo kati ya nchi mbili hizo kutokana na utendaji wake wa kazi.Kwa upande wa Zanzibar, Dk. Shein alimueleza Balozi Haule kuwa kumekuwa na uhusiano wa kidugu na kihistoria kati ya nchi hiyo na Zanzibar hasa ikizingatiwa uhusiano kati ya Zanzibar na Mombasa katika nyakati za ukoloni hatua ambayo imepelekea kuimarika kwa uhusiano huo hadi hii leo na kuweza kuwepo kwa Ubalozi Mdogo huko mjini Mombasa. Dk. Shein alisema kuwa hivi sasa Kenya na Zanzibar kumekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri wa kibiashara hasa katika zao la karafuu, ambapo wafanyabiashara wa nchi hiyo wamekuwa wakinunua karafuu kupitia Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).Alisema kuwa hatua hiyo imeweza kuondosha tatizo lililokuwepo hapo siku za nyuma ambapo biashara hiyo ilikuwa ikifanywa kimagendo na baadhi ya watu kati ya Kenya na Zanzibar na kuikosesha Zanzibar kuimarisha pato lake la uchumi. Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi Haule haja ya kulitangaza soko la Utalii nchini Kenya kwani nchi hiyo nayo imeweza kupata mafanikio katika sekta hiyo. Nae Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya Mhe. John Michael Haule alimuahidi Dk. Shein kuwa katika utekelezaji wa Kazi zake nchini humo atazidi kujenga uhusiano na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya.Balozi Haule alieleza kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo utaimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati katika kuhakikisha Sera ya Demokrasia ya Uchumi kati ya pande mbili hizo inaimarishwa. Katika mazungumzo yake Balozi huyo, alisisitiza haja ya kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Utalii hapa nchini sambamba na kuimarishwa kwa usafiri kati ya Kenya na Tanzania ikiwemo Zanzibar ili kutoa usafiri wa uhakika kwa wageni wanaotembelea vivutio vya kitalii vilivyopo katika maeneo hayo.Aidha, Balozi huyo aliahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano katika nyanja ya uwekezaji na biashara hasa ikizingatiwa kuwa katika nchi za Afrika ya Mashariki nchi ya Kenya inaongoza kwa wawekezaji na wafanyabiashara wake kuekeza hapa Tanzania. Pamoja na hayo, mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha mambo mbali mbali ya kimaendeleo yakiwemo ya kiuchumi kati ya Kenya na Tanzania.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo