Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Mji Mkongwe kutumia njia moja ( One Way Traffic)
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuanzisha utaratibu wa kutumia njia ya upande mmoja kubwa ya kuingia Mji Mkongwe kuanzia tarehe nane mwezi huu ili kupunguza usumbufu unaowapata wageni na watumiaji wengine wa Mji huo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mamlaka ya Mji Mkongwe Forodhani, Mkurugenzi Mkuu Issa Saidi Makarani amesema uwamuzi huo umefikiwa kutokana na ongezeko kubwa la vyombo vya moto linalohatarisha usalama wa mji huo ambao ni urithi wa kimataifa. Amesema mji wa Zanzibar umekuwa ukipokea watalii na wageni wengi na wakati wa matembezi yao wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kutokana na kuongezeka vyombo hivyo. Ameongeza kuwa ongezeko hilo la magari pia limepelekea athari kubwa kwenye majengo kutokana na mtikisiko mkubwa wa magari yenye uzito mkubwa na kubomoa baadhi ya majengo ya mji. “Watumiaji wa Mji huu na wanaofika kila siku kwa shughuli zao za kimaisha wanapata usumbufu na kubwa zaidi wingi wa vyombo hivyo tayari vimesababisha athari ya baadhi ya majengo,”alisisitiza Mkurugenzi Makarani. Amesema njia kubwa ya ndani ya kuingilia Mji Mkongwe itaanzia Vuga kupitia Afrika House , Hoteli ya Serena , Wizara ya Ardhi , Makaazi, Maji na Nishati , Benki ya NBC , Jengo La zamani la Watoto Forodhani , njia ya Mizingani hadi kuishia lango kuu la kuingia bandarini Malindi. Amezitaja njia zitakazofungwa kuanzia tarehe nane kuwa ni ile inayoanzia jengo la Wizara ya zamani ya Mawasiliano na Uchukuzi kupitia Kiponda na kumalizikia Darajani, njia inayoingia Mkunazini na kumalizikia Skuli ya Sunni Madrassa na njia inyozunguka nyuma ya jengo la sinema ya zamani Majestic. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis amesaema lengo la kuweka zoezi hilo ni kuweka usalama kwa wenye magari na wanaokwenda kwa miguu. Amewaomba wananchi kuunga mkono zoezi hilo ambalo litaweka mji Mkongwe katika hadhi na ubora wake uliopelekea kuwa miongoni mwa Miji ya Urithi wa kimataifa duniani. Mkurugenzi wa Baraza la Manispaaa Aboud Hassan Serenge amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya Mji Mkongwe kubadilika na kuanzisha utamaduni wa kuimarisha suala la usafi.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo