Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Zec yamtangaza mshindi Dk..Shein,nae ahaidi kuongeza kasi ya maendeleo Zanzibar.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC imemtangaza mgombea nafasi ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4 ya kura zote halali. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana katika ukumbi wa Salama huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar leo, Mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha alisema jumla ya wapiga kura waliojitokeza ni 341,865 sawa na asilimia 67.9 ya watu 503,580 waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura. Kati ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa ZEC,kura 13,538 sawa na asilimia 4.0 ziliharibika.Kutokana na matokeo hayo Dk. Shein ameweza kutetea tena nafasi yake hiyo hivyo kumuwezesha kuiongoza Zanzibar kwa kipindi kingine cha miaka mitano hadi mwaka 2020. Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kushirikiana kuijenga Zanzibar na kuendelea kuling’arisha jina la Zanzibar mbele ya macho ya ulimwengu kwa sifa zake na historia yake.“Katika kipindi kijacho cha miaka mitano tutajitahidi kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwa kutumia rasilimali zetu tulizonazo na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za maendeleo zinazotukabili” Dk. Shein alisema. Aliwaeleza mamia ya wananchi wakiwemo wanachama na washabiki wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo kuwa uongozi wake kama ulivyokuwa katika kipindi kilichopita utazingatia haki na kusisitiza kuwa hatavumilia kuona mtu akidhumuliwa haki yake.“Nitajitahidi kutenda haki kwa kila mwananchi kwa kuzingatia Sheria na Katiba” alisema na kusisitiza kuwa nia yake ni “moja tu kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar” Dk. Shein aliieleza hadhara hiyo ambayo ilijumuisha kundi kubwa la waandishi wa habari kutoka vyombo vya humu nchini na nje ya nchi kuwa anaelewa uzito wa nafasi hiyo ya urais na kwamba anafahamu namna ya kuanza na kumalizia.Aliwashukuru wananchi wote waliomchagua na wasiomchagua kwa kuwa wote wametekeleza haki yao ya kidemokrasia nan kueleza kuwa hiyo ni heshma kubwa kwake na ahadi yake kwa wananchi hao ni kutimiza wajibu wake wa kuwaletea maendeleo. Dk. Shein alirejea shukrani kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa kumuamini na kumteua tena kugombea nafasi hiyo na kusisitiza kuwa Serikali atakayoiunda itasimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kama ilivyonadiwa wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza tena. Katika maelezo yake hayo Dk. Shein alimshukuru Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Rais John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha nchi inakuwa katika amani na utulivu wakati wote na pia alivipongeza vyombo hivyo kwa kuhakikisha usalama wakati wote wa uchaguzi. “wako waliotaka Zanzibar iingie katika machafuko…wako waliokuwa wakifanya uchichezi kupitia mitandaoni na visa vingi mitaani lakini wameshindwa” alieleza Dk. Shein.Aliwapongeza wagombea wa vyama vingine vilivyoshiriki mbio hizo za kuwania nafasi ya urais kwa kushiriki kwao na pia kuwashukuru wanachama na wapenzi wa vyama hivyo kwa kutumia haki yao ya kidomkrasia.Alitoa pongezi na shukrani maalum kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na watendaji wake kwa kuweza kuandaa na kufanikisha uchaguzi hadi matokeo kutangazwa na kuongeza kuwa “Tunaelewa ugumu wa kazi hiyo na mnastahiki pongezi”
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo