Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Makabidhiano ya Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Khalid Salum Mohammed amesema kuwa Tume ya Mipango ina jukumu kubwa katika kufikia lengo na dhamira ya Serikali katika kipindi hiki cha pili cha Awamu ya Saba katika kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato sambamba na ukuaji wa uchumi. Aliyasema hayo, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi ya Tume ya Mipango kati yake na Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Tume hiyo iliyopo Vuga mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyejiti wa Baraza la Mapinduzi. Waziri Khalid akinukuu hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Kohamed Shein, aliyoitoa Katika uzinduzi wa Baraza la Tisa la Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid alisema kuwa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato na kasi ya ukuaji uchumi aliyoeleza Rais itafikiwa kutokana na kujenga mashirikiano ya dhati kwa viongozi na wafanyakazi wote. “Malengo yote hayo mawili yatafikiwa iwapo kutakuwa na mashirikiano ya kutosha likiwemo lengo la kuhakikisha kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi inafikia asilimia 8-10 katika miaka mitano ijayo na lile la kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka TZS bilioni 362.8 mwaka 2014/2015 hadi kufikia TZS bilini 800 ifikapo mwaka 2020/2021”,alisema Dk. Khalid. Katika maelezo yake Dk. Khalid alisisitiza haja ya kufanya kazi kwa kujitolea kwa kila mfanyakazi na katika kila sehemu aliyopo achape kazi kwani hayo ndio matarajio ya Mhe. Rais pamoja na wananchi katika kuiletea Zanzibar maendeleo endelevu. Waziri Khalid alisema kuwa rasilimali fedha ni muhimu na sekta zote za Serikali zinategemea sana usimamizi na ugawaji wa rasilimali hizo hivyo Tume ya Mipango ina jukumu kubwa katika kusimamia hilo na kuhakikisha linafanikiwa. Dk. Khalid aliahidi kuimarisha zaidi mashirikiano kati yake, viongozi na watendaji wote wa Tume hiyo ambayo hapo kabla ilikuwa chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora kwa lengo la kufikia matarajio ya wananchi katika kuwaletea maendeleo endelevu. Aidha Waziri Khalid alimuhakikishia Mhe. Dk. Mwinyihaji kuwa ataendelea kushirikiana nae samba na kuchota hazina ya uzoefu, mawazo, busara na hekima alizonazo katika utendaji wake wa kazi huku akiahidi kuwa hatoacha kujifunza kutoka kwa watendaji na viongozi wa Tume hiyo ya Mipango. Sambamba na hayo, Dk. Khalid alisisitiza haja kwa viongozi na watendaji wa Tume hiyo kuimarisha zaidi mawasiliano miongoni mwao pamoja na kupeana taarifa zilizosahihi. Mapema Dk. Mwinyihaji Makame ambaye katika Kipindi cha kwanza katika uongozi wa Awamu ya Saba alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora aliwataka watendaji na viongozi wa Tume hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa Waziri huyo mpya kama walivyompa yeye katika uongozi wake. Dk. Mwinyi aliwahakikishia watendaji wa Wizara pamoja na Tume hiyo kuwa wamepata Waziri mchapa kazi na hodari na mwenye kasi katika utendaji wake wa kazi hivyo wakimpa mashirikiano ya kutosha anaamini kuwa mafanikio makubwa yatapatikana katika kuiletea maendeleo Zanzibar. Dk. Mwinyi alisema kuwa Tume ya Mipango ndio roho ya nchi, kwani ndio inayotoa maelekezo ya matumizi na mipango yote ya kifedha serikalini hivyo kuwepo mashirikiano katika uongozi wa Tume hiyo kutafikia malengo yaliowekwa katika kuiimarisha Zanzibar. Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya watendaji wa Tume ya Mipango, Bi Sharifa Abdalla Khamis aliahidi kuwa wafanakazio wote wa Tume hiyo watampa mashirikiano makubwa Waziri wao huyo mpya huku wakiahidi kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo