Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
China Kuiunga Mkono Zanzibar Uthibitisho wa Muendeleo wa Uhusiano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo cha Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kuonyesha muelekeo wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar ni uthibitisho wake wa muendelezo wa uhusiano iliyokuwa nao kati yake na Zanzibar. Balozi Seif alisema hayo nyumbani kwake Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akizungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi sita wa Mahakamu Kuu ya China. Balozi Seif alisema China ni nchi ya kwanza iliyoamua kuiunga mkono Zanzibar mara tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa marejeo uliofanyika Tarehe 20 Machi mwaka huu katika hali ya amani na utulivu. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Nchi hiyo kubwa ya Bara la Asia kwa jitihada zake ilizochukuwa katika kuweka mfumo maalum wa utoaji wa mafunzo kwa watendaji wa Taasisi za Umma kwa nchi zinazoendelea kiuchumi ikiwemo Tanzania. Balozi Seif alisema utaratibu huo kwa kustawisha uwajibikaji na uchumi umesaidia zaidi watumishi wanaopata mafunzo nchini China kuwa na uwezo wa utekelezaji wa majukumu yao kitaaluma zaidi. “Tumefarajika sana jinsi ya watendaji wa Baraza la Wawakilishi, Waheshimiwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanavyoitumia fursa hiyo ya mafunzo kwa kuwajibika kitaaluma wakati wa kuwatumikia wananchi ”. Alisema Balozi Seif. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Jaji Mkuu huyo wa Mahakama Kuu ya China na Ujumbe wake kwamba uhusiano uliopo wa kihistoria katika ya pande hizo mbili utadumishwa zaidi kwa faida ya wananchi wake. Mapema Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Watu wa Chima Mheshimiwa Zhang Giannan akiambatana pia na Balozi Mdogo wa China aliyepo hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang alisema wananchi wa taifa hilo la Bara la Asia wanafurahia kuona uhusiano wa Nchi hiyo na Zanzibar bado unaendelea kudumu. Jaji Giannan alieleza kwamba Mikakati ya China katika hatua yake ya baadaye imepanga kuimarisha zaidi uhusiano wake na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla katika Sekta za Utamaduni, sanaa pamoja na Michezo. Alisema eneo hilo kwa sasa ni muhimu katika dhana ya kuwaunganisha Vijana ambao ndio kundi kubwa katika jamii kuelekeza nguvu zao katika sekta hizo zenye nafasi pana ya kutoa fursa za kujitegemea badala ya kusubiri Serikali ambazo tayari zimekuwa na ufinyu wa nafasi za ajira. Ujumbe huo wa Mahkama Kuu ya Jamuhuri ya Watu wa China upo Nchini kufanya ziara ya kutathmini maendeleo ya ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hiyo na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo pia Zanzibar.
Official Reports
A Bill for an Act to repeal the Zanzibar Electoral Commission Act, No. 9 of 1992-Date Posted: 17-02-2017
Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Tume ya Uchaguzi Nam, 9 ya 1992-Date Posted: 17-02-2017
HOTUBA YA MAONI YA KAMATI YA KUSIMAMIA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA KUHUSIANA NA MSWADA WA SHERIA YA KUFUTA SHERIA YA TUME YA UCHAGUZI NAM.9 YA 1992 NA KUTUNGA SHERIA YA KUANZISHA AFISI YA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR-Date Posted: 17-02-2017
HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. AL HAJJ DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA BARAZA LA IDD EL FITRI JULAI, 2016 (1 SHAWWAL, 1437)-Date Posted: 07-07-2016
Hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa Fedha 2016/2017. -Date Posted: 20-05-2016

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo