Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wafanakazi msigeuze sehemu za kazi kuwa majukwaa ya siasa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wafanyakazi nchini kutozigeuza sehemu za kazi kuwa majukwaa ya kisiasa badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kasi ya maendeleo.Sambamba na kauli hiyo amewaonya watumishi wa Serikali dhidi ya vitendo vya ubaguzi katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kuwatahadharisha juu ya vitendo vya aina hiyo kuwa havitavumiliwa. Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani leo yaliyofanyika katika hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, Dk. Shein alisisitiza umuhimu wa kuwajibika na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayeshindwa kuwajibika katika eneo lake la kazi. “wakati tulio nao si wakati wa maneno,sasa ni wakati wa vitendo. Jukumu letu ni kuipeleka mbele nchi yetu ili ifikie nchi yenye uchumi wa kati” alisema Dk. Shein na kuongeza kuwa hilo linawezekana kwani hatua iliyofikiwa hadi sasa ni nzuri. Alifafanua kuwa ni lazima watumishi wawe wabunifu na kujisimamia wenyewe badala ya kungoja kusimamiwa na kusukumwa katika mambo yaliyo ndani ya uwezo wao.Kwa upande wa viongozi alisema kwa watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao serikali haitakuwa na jingine bali kuwachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo. Kuhusu maslahi ya watumishi Dk. Shein aliwaeleza mamia ya wafanyakazi waliohudhuria maadhimisho hayo kuwa Serikali itaendelea kutekeleza ahadi zake za kuimarisha maslahi yao na kufafanua kuwa ahadi ya kuongeza mshahara wa kima cha chini hadi shilingi laki tatu inafanyiwa kazi.Sambamba na utekelezaji wa ahadi hiyo, aliahidi serikali kuyangalia upya mafao na posho nyengine za watumishi ili ziende na wakati kadri hali ya uchumi itakavyoimarika. “…tutafanya kila tuwezalo ili tulipe viinua mgongo kwa wakati na tulipe malimbikizo ya malipo ya wafanyakazi, hasa walimu” Dk. Shein alieleza huku akisisitiza kuwa haki ya watumishi hao lazima zitalipwa na kuahidi serikali kuandaa utaratibu bora zaidi wa kuhakikisha madeni hayo yanalipwa.Aidha, Mheshimiwa Rais alibainisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ili kuhakikisha kuwa haki na maslahi ya wafanyakazi yanaendelea kuimarishwa kwa kuzingatia sheria za Zanzibar na Mikataba ya Kimataifa. Kuhusu kuimarisha majadiliano Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha utaratibu wa majadilianao ya pamoja kazini kwa minajili ya kuimarisha uhusiano bora na kuondoa mizozo katika sehemu za kazi ili kuleta ufanisi.Katika kufaya hivyo alieleza kuwa serikali imehakikisha vyombo vyote vya majadiliano kati ya waajiri na waajiriwa vimeundwa na vinafanyakazi ipasavyo. Kwa upande wa kuundwa kwa chombo cha kitaifa cha majadilianao alitoa wito kuwataka wawakilishi wa wafanyakazi wanaoingia katika vikao hivyo kuitumia fursa hiyo kwa kuwasilisha hoja zenye kuzingatia maslahi ya wafanyakazi na jamii kwa jumla.Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais wa Zanzibar alieleza dhamira ya serikali ya kuhakikisha inatekeleza vipaumbele vyake huku akirejea wito wake wa kuzitaka wizara na taasisi za serikali kujiepusha na matumizi yasiyo ya lazima. “Tmedhamiria kubana matumizi ikiwemo kwa kupunguza safari za nje na za ndani. Wako baadhi ya watumishi wanaomba kualikwa ili wasafiri. Hatuko tayari kuona jambo hili katika kipindi hiki” Dk. Shein alisisitiza. Kwa upande wake Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauldine Castico alisema amefurahishwa na uhusiano mzuri ulipo kati ya serikali, waajiri na waajiriwa.Alibainisha kuwa kumekuwepo na ushirikishwaji mkubwa katika masuala mabalimbali yanayohusu wafanyakazi matoeo yake ni kupungua kwa misuguano na migongano mikubwa katika kazi na suala la maslahi. Kwa hivyo aliahidi kuendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapewa fursa ya kusilikilizwa na changamto zao kutaliwa.Katika maadhimisho hayo Shirika la Kazi Duniani (ILO), Jumuiya ya Waaajiri (ZANEMA) na ZATUC zilitoa salamu zao kuadhimisha siku hiyo muhimu na yenye historia kubwa ya harakati za wafanyakazi za kudai haki na maslahi yao.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo