Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Mhe:Dk.Shein,amwambia Magufuli wananchi wa Zanzibar wako pamoja nae.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemhakikshia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli kuwa wananchi wa Zanzibar wako pamoja nae katika harakati za kuijenga Tanzania. Akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Magufuli katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika huko katika kiwanja cha Gombani wilaya ya Chake mkoa wa Kusini Pemba leo, Dk. Shein alisema tangu Chama cha Mapinduzi kiliposhika madaraka baada ya uchaguzi mkuu serikali zake zimeanza vizuri na wananchi wategemee mambo mazuri zaidi. Mhe:Dk.Shein,amwambia Magufuli wananchi wa Zanzibar wako pamoja nae. “tangu tulipoapishwa tumeanza vizuri na sisi tunafahamiana tulifanya kazi pamoja vizuri na tutafanya vizuri zaidi” alieleza Dk. Shein na kutoa wito kwa wananchi kuzidi kuwaamini yeye na Dk. Magufuli. Kadhalika Dk. Shein alirejea utayari wake wa kushirikiana benga kwa bega na Rais Dk. Magufuli katika kusimamia amani na utulivu nchini pamoja na kuuenzi, kuulinda na kuuimarisha Muungano ulioanzishwa na waasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. “Tulipokuja hapa mwaka jana kuomba kura sote wawili tulikuja na mambo mawili makubwa ambayo ni kuimarisha Muungano wetu na kusimamia amani na utulivu wa nchi yetu” Dk. Shein aliwaeleza maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo. Dk. Shein aliahidi kuongeza nguvu katika kuimarisha Muungano ambapo alibainisha kuwa kwa sasa zile kinazoitwa kero za Muungano zimebaki chache na kwamba pande zote mbili za Mungano huo ziko tayari kukabiliana na changamoto mpya za zinazoweza kujitokeza. Aliongrza kuwa amani na utulivu wa nchi yetu ndio nguzo ya Muungano wa watanzania na nguzo ya maendeleo yetu na kusisitiza kuwa hakuna mbadala wa amani ya nchi. Kwa hivyo alimhakikishia Rais Dk. Magufuli kuwa atatumia kila uwezo alionao na kutoa ushirikiano utakiwao katika kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa kisiwa cha amani. “Nia yetu ni moja, kuipeleka nchi yetu katika maendeleo. Wananchi naomba waendelee kutuamini na tutaendelea kuhakikisha kuwa wanaishi kwa amani na utulivu katika nchi yetu” alisisitiza Dk. Shein. Dk. Shein alimpongeza Dk. Magufuli kwa kutekeleza Ilani kwa kasi kubwa na kubainisha kuwa wananchi wanathamini kazi yake na kwamba CCM kumteua Dk. Magufuli kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa uamuzi sahihi. “Una kila sababu ya kufika hapa tena leo kuwaona na kuzungumza na ndugu zako wa Pemba kueleza tena dhamira yako ya kuwatumikia na wao wana haki kukusikiliza na kufuata maelekezo na ushauri wako” Dk. Shein alieleza. Katika mkutano huo Dk. Magufuli aliwataka wananchi wa Zanzibar kuelewa kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba kazi iliyo mbele yao ni kufanyakaiz na kujenga nchi. Dk. Magufuli ambaye yuko Zanzibar kwa ziara ya siku mbili aliwashukuru na kuwapongeza wananchi wa Pemba kwa mapokezi makubwa pamoja na kuhudhuria mkutano wake huo bila ya kujali itikadi za vyama vyao. Dk. Magufuli aliondoka Pemba baadae jioni kwenda Unguja ambapo kesho anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo