Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Mhe:Dk. Shein katemebelea uwanja wa Gombani.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekagua matengenezo makubwa ya kuwekwa mpira wa kukimbilia (Tatan) katika uwanja wa Gombani Pemba na kupongeza hatua iliyofikiwa ambayo itazidi kuimarisha sekta ya michezo hapa nchini.Dk. Shein alifika kiwanjani hapo akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma ambaye alimpa maelezo ya kina juu ya maendeleo ya matengenezo hayo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katika ukaguzi wake huo, Dk. Shein alisema kuwa kukamilika kwa uwekaji huo wa Tatan katika uwanja huo wa Gombani Pemba kutauwezesha mchezo wa riadha kufanyika kwa ustadi mkubwa zaidi sambamba na kuufanya uwanja huo uwe umekamilika kimichezo hatua ambayo itaendeleza kuibua vipaji vya mchezo huo hapa nchini.Alisisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi za kuimarisha na kuongeza miundombinu ya michezo katika maeneo yote yaliotengwa maalum kwa michezo katika visiwa vya Unguja na Pemba ili kuirejesha Zanzibar katika asili yake kwenye anga ya michezo.Pamoja na hayo, Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi wa Wizara hiyo kuhakikisha eneo lote lililozunguka uwanja huo linakuwa salama na halivamiwi kwa ujenzi usio rasmi. Nae Waziri wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma alimueleza Dk. Shein maendeleo yaliofikiwa katika matengenezo ya tatan katika uwanja huo wa Gombani pamoja na hatua nyengine zinazoendelea kuchukuliwa ili uwanja huo uzidi kuvutia kimataifa.Aidha, Waziri Juma alieleza kuwa hatua iliyofikiwa katika matengenezo hayo ni nzuri na kumuhakikishia Dk. Shein kuwa juhudi zaidi zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha baadhi ya maeneo ya uwanja huo yanafanyiwa ukarabati awamu kwa awamu yakiwemo maeneo ya majukwa ili uzidi kuimarika na kuvuti zaidi. Matengenezo ya uwekaji wa tatan hizo yalioanza mwaka 2013 yalifanyika kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza na ya pili ilifanywa na Kampuni ya Nowe Investment kutoka Dar-es-Salaam na awamu ya pili ya uwekaji wa tatan ilifanywa na Kampuni ya Guangzhou Jrace Athletic kutoka China.Tatan hiyo iliyozungushwa katika kiwanja hicho mbali ya kuwekwa katika sehemu maalum kwa kukimbilia pia imeongezwa kwa baadhi ya maeneo katika kiwanja hicho ambayo yatawezesha baadhi ya michezo kuweza kuchezwa katika kiwanja hicho ukiwemo mchezo wa vinyoya na michezo mengineyo. Hata hivyo, uwanja huo wa Gombani tayari umeshawekewa nyasi za bandia ambazo tayari zimeshaanza kutumika kwa kuchezewa mashindano mbali mbali ya mpira wa miguu yanayofanyika kisiwani Pemba.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo