Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Mhe.Dk.Shein aipongeza Ofisi ya Rais na MBLM na kuhimiza ushirikiano katika utekelezaji majukumu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na ukamilishaji vikao vya kupitisha Mipango ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 vilivyoanza wiki iliyopita.Katika kikao hicho Dk. Shein aliwapongeza viongozi na watendaji wa Ofisi hiyo kwa kufanyakazi kwa ushirikiano (team work) ambao alisema umekuwa msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi. Mhe.Dk.Shein aipongeza Ofisi ya Rais na MBLM na kuhimiza ushirikiano katika utekelezaji majukumu Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Awamu ya Saba, Ofisi hiyo ilitekeleza vyema majukumu yake ya kutekeeleza Ilani lakini ametoa wito kwa viongozi na watumishi kuongeza kasi katika kipindi hiki cha pili cha Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa mwaka 2015-2020. Katika mnasaba huo ameitaka Ofisi hiyo kuhakikisha kuwa kila idara ya Ofisi hiyo inakuwa na watumishi wa kutekeleza majukumu ya idara kisiwani Pemba ili kuwe na uwiano sahihi wa utekelezaji wa Ilani Unguja na Pemba. Katika hatua nyingine Dk. Shein ameitaka Kurugenzi ya Mawasilianao Ikulu kubuni njia nyingi na rahisi zaidi za kuwasiliana na wananchi ili kuendelea kuwaweka karibu Serikali.Dk. Shein amebainisha kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa kuwapatiwa wananchi taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za serikali kupitia njia mbalimbali za mawasiliano lakini ipo haja ya kubuni njia nyingine rahisi ambazo zitapanua wigo wa mawasiliano kati ya Serikali na wananchi.Alisisitiza kuwa taarifa muhimu za Serikali hazina budi kuwafikia wananchi kwa wakati na kwa uhakika ikiwezekana kutumia mfumo wa utawala kupitia kwa masheha ambapo baadhi ya machapisho yanaweza kuwasilishwa kwao na kugawanywa kwa wananchi. Katika kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alihimiza pia kuharakishwa kwa mchakato wa matayarisho ya Sera ya Diaspora ili iweze kutumika kwa faida ya wanadispora na nchi kwa jumla. Akizungumza wakati wa majumuisho ya kikao hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu alimshukuru mheshimiwa Rais na viongozi wengine waliohudhuria kwa michango yao na kuahidi kuzingatia ushauri wao ili kuboresha mpango huo kwa minajili ya kufikia malengo yaliyowekwa. Aidha Waziri Gavu alieleza kuwa mchakato wa kuunda Sera ya Diaspora umo katika hatua za mwisho kukamilika baadaya kupitishwa katika Kikao cha Makatibu wakuu na kwamba hivi sasa inasubiri kuwasilishwa katika Baraza la Mapinduzi hivi karibuni. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee. Vikao vya kupitisha Mipango ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 -2020 vilianza Jumatatu tarehe 5 Septemba, 2016 ambapo kikao cha kimehitimisha idadi ya wizara 13 ziliwasilisha mipango yao na kujadiliwa.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo