Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Serikali itahakikisha maslahi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari yanaboreshwa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa mazingira ya kazi pamoja na maslahi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari vya serikali yanaimarishwa ili kurejesha hadhi ya taasisi hizo. Dk. Shein ambaye alivitembelea vyombo vya habari vya Redio pamoja na gazeti la Zanzibar Leo na kufanya mahojiano maalum na Shirika la Habari na Utangazaji Zanzibar ZBC, alisema ameridhishwa na utendaji wa kazi wa viongozi na wafanyakazi wa vyombo hivyo ambao amesema, wamekuwa wakijitahidi kufanya kazi vizuri licha ya changamoto kadhaa wanazokabiliana nazo. Amesema Serikali imedhamiria kulifanyia marekebisho makubwa Shirika la Habari na Utangazaji Zanzibar na vyombo vyote vya habari vya Serikali sio tu kwa kuinua viwango vya mishahara ya wafanyakazi, lakini vile vile kuweza kutoa tuzo maalum kila inapohitajika kufanya hivyo kwa wafanyakazi watakaofanya kazi zao vizuri kuinua ari na motisha wa wafanyakazi. Ameongeza kuwa mchakato unaendelea wa kutayarisha na hatimaye kurejesha miundo ya utumishi “scheme of service” ambayo kwa kiasi kikubwa nayo iterejesha heshima ya kazi ambayo ilionekana kupungua siku za hivi karibuni ikilinganishwa na miaka iliyopita wakati ilipokuwa ikitumika vyema. Amefahamisha kuwa katika hatua za awali kuelekea kuziimarisha taasisi za vyombo vya habari vya Serikali, Serikali imeshatoa agizo kuitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuandaa posho maalum kwa wafanyakazi ambao wanajulikana kuwa wanafanyakazi katika mazingira magumu. Akizungumzia baadhi ya wafanyakazi ambao wameondoka kwenye vyombo vya habari vya Serikali kutokana na maslahi duni na mazingira yasiyoridhisha, Rais wa Zanzibar alisema ana matumaini makubwa kwamba wengi miongoni mwa wafanyakazi hao wataweza kurejea siku zijazo kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine wengi kwenye taasisi mbali mbali. “nyumbani ni nyumbani, naamini iwapo tutaimarisha mazingira bora ya kazi watarejea, wengi tumewaona wakirejea kutokana na mapenzi yao na nyumbani” alisema. Amesema pamoja na ukweli kwamba katika kipindi cha kwanza cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya saba ilifanya mabadiliko makubwa ya mishahara ambayo hayajawahi kufanywa kabla, wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao kwao bado viwango hivyo vya mishahara havijawaridhisha sana. Hata hivyo Dk. Shein alielezea matumaini yake kwamba katika kipindi cha miezi sita au saba ijayo, hali ya vyombo vya habari vya Zanzibar itabadilika na kwamba watu wengi watavutiwa kufanyakazi kwenye vyombo hivyo. Kuhusu gazeti la Zanzibar Leo, Rais wa Zanzibar alisema Serikali imeshanunua mitambo mipya ya kisasa ya uchapishaji ambayo itatumika pia, kuchapishia gazeti hilo badala ya kuchapishwa nje ya Zanzibar, jambo linalosababisha mrundikano mkubwa wa deni la gharama za uchapishaji. Nao wafanyakazi na watendaji wa vyombo hivyo vya habari walitoa pongezi zao za dhati kwa Dk. Shein kwa kufanya ziara yake hiyo ya hafla ya kuwatembelea pamoja na kuwasikiliza changamoto walizonazo. Jumamosi iliyopita, Rais wa Zanzibar alikutana na uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Uongozi wa Shirika la Habari na Utangazaji Zanzibar (ZBC) pamoja na Uongozi wa Zanzibar Leo kuzungumzia njia ambazo zatasaidia kuimarisha zaidi matangazo ya Redio na TV za Shirika la Habari na Utangazaji Zanzibar – ZBC. Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo