Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Rais Dk Shein atoa miezi miwili jengo la Ofisi ya Zimamoto likamilike
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa miezi miwili kwa Taasisi zote zinazohusika na ujenzi wa ofisi ya Zimamoto zinazojengwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar ziwe zimeshakamilisha ujenzi huo. Dk. Shein alitoa agizo hilo mara baada ya kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Zimamoto huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, ambapo ujenzi huo unaonekana kusuasua kwa muda mrefu. Kutokana na kusuasua kwa ujenzi huo ndipo kulikompelekea Dk. Shein kutoa agizo hilo kwa Taasisi zote husika kukamilisha ujenzi huo ndani ya kipindi hicho hasa ikizingatiwa kuwa wahusika walipewa agizo hilo mwezi Mei mwaka jana wakati Mheshimiwa Rais alipofanya ziara kutembelea uwanja huo. Dk. Shein alisema kuwa tokea kipindi hicho hadi leo bado ujenzi huo haujaanza na kusisitiza ni lazima ukakamilike katika kipindi hicho hasa ikizingatiwa kuwa tayari serikali imeshatoa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 3.5 kwa ajili ya ununuzi wa gari za zimamoto pamoja na dola milioni 1.5 ambazo zimetolewa na Benki ya dunia kwa ajili ya nununuzi wa gari hizo. Dk. Shein alisisitiza kuwa tarehe kama ya leo mwezi wa Disemba mwaka huu atarudi tena kwa ajili ya kuangalia jengo hilo likiwa limekamilika kwani anatambua kuwa Serikali ina fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi huo ila kuna changamoto ndani ya taasisi hizo zinazokwaza utekelezaji wa agizo lake. “Tusifanye kazi kwa utamaduni tuliozoea, nimekupeni muda mrefu miezi miwili, malizeni mkimaliza nitakuja, hamkunialika nitakuja mkinialika nitakuja…pesa zipo lakini hamjaziomba”,alisema Dk. Shein. Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutakuwa na tija kubwa Serikali hasa ikizingatiwa kuwa ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja huo linatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Nae Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Khair alimueleza Dk. Shein haja ya kuwepo kwa mashirikiano kati ya taasisi zote zinazosimamia ujenzi huo hasa kwa upande wa Wizara ya Mawasiliano, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Idara ya Zimamoto ili kufanikisha jukumu hilo. Mapema Kamishna wa Idara ya Zimamoto Zanzibar Ali Abdalla Malimosi alimueleza Dk. Shein changamoto mbali mbali zinazoikabili kikosi hicho katika eneo hilo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. Wakati huo huo, Dk. Shein alifika Mbweni kukagua eneo la mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na kupongeza juhudi zinazochukuliwa na Mfuko huo katika kuimarishaji miradi mbali mbali ya maendeleo yenye tija. Dk. Shein alisema kuwa ndani ya miaka sita ya uongozi wake, Mfuko huo umeweza kufanya vizuri kwa kuanzisha miradi kadhaa ukiwemo ujenzi wa viwanja vya kufurahishia watoto Kariakoo Ungujua na Tibirinzi Pemba, ujenzi wa mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi, pamoja na ujenzi wa jumba la treni unaotarajiwa kuanza mwezi ujao. Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa ujenzi huo wa nyumba za kisasa una faida kubwa ambao unatarajiwa kuwa na nyumba 252 zikiwemo za vyumba vitatu, viwili na vinne. Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Abdulwakil Haji Hafidh alimueleza Dk. Shein kuwa ujenzi huo wa majengo 18 ya ghorofa unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2018 na unatarajiwa kugharimu Tsh. bilioni 43. Mkurugenzi huyo alieleza kuwa mradi huo utakuwa na Mabloki 18 ya Majengo ya Ghorofa Saba zenye Fleti 252 ambao utajengwa kwa awamu tatu tofauti ambapo tayari wameshaanza kujenga Mabloki Matano yenye Nyumba 70. Alieleza pia kuwa tayari kwa hatua za awali shirika limeshatumia shilingi bilioni 8 ambapo tayari ujenzi huo ukiwa unaendelea nyumba 55 zimeshapata wanunuzi kutoka sehemu mbali mbali na hivi sasa wanafunga mikataba nao. Mkurugenzi Mtendaji huyo alieleza kuwa mradi wa nyumba za Mbweni mwanzoni ulipangwa kwa ajili ya wananchi wenye vipato vya kati na chini ambazo zitauzwa kati ya shilingi milioni 168 hadi 249 lakini imebainika kuwa watu wengi hawatazimudu hivyo Mfuko umeamua kujenga za kipato cha chini huko eneo la Tunguu. Alibainisha kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo unaojumuisha ujenzi wa magorofa matano itakamilika mezi Aprili mwakani na kufuatiwa na ujenzi wa magorofa mengine 8 katika awamu ya pili na awamu ya tatu ni ya ujenzi wa magorofa yatakayo baki. Alieleza kuwa tayari wameshaanza kutafuta wanunuzi na wameshatembelea sehemu mbali mbali za ndani na nje kwa ajili ya kujitangaza huku akimueleza kuwa nyumba hizo zitakuwa na maeneo ya huduma muhimu yakiwemo maduka pamoja na ukumbi mkubwa wa kisasa ambao utajengwa katika eneo hilo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa juhudi za makusudi zimefanywa katika kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo unakuwa imara zaidi chini ya Kampuni ya ujenzi ‘Dezo Civil Construction Limited yenye makao makuu yake Jijini Dar-es Salaam. “Ujenzi wetu tumeupanga kuutekeleza kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza tutajenga Bloki Tano, ile ya Pili pia tutajenga Bloki Tano na ya mwisho tutamalizia kwa Bloki Nane “, alisema Mkurugenzi huyo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar. Akitoa maelezo wakati akimtembeza kwenye ujenzi wa nyumba hizo Meneja Mipango,Uwekezaji na Utafiti wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Khalifa Muumin Hilal alimuhakikishia Dk. Shein umadhubuti mkubwa wa nyumba hizo. Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo