Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wizara ya Elimu kuwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja ya kujitegemea kwa kuwatumia wataalamu waliopo nchini sambamba na kutumia nyenzo na rasilimali zilizopo ili kupunguza gharama zisizo za lazima na hatimae kuweza kuisaidia Serikali. Dk. Shein aliyasema hayo, Ikulu mjini Zanzibar katika kikao maalum kati yake na uongozi wa Wizara ya Elimu mara baada ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka 2016. Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa kuna faida kubwa iwapo wataalamu waliopo Mawizarani watatumiwa vizuri badala ya wataalamu kutoka nje ya nchi. Alisema kuwa kwa upande wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imejaaliwa kuwa na wataalamu wa fani mbali mbali ambao wanaweza kuisaidia Wizara hiyo katika kufanya mambo yake mbali mbali katika kuimarisha sekta ya elimu. Aidha, Dk. Shein alieleza juhudi za makususdi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukusanyaji wa mapato huku akisisitiza azma ya Serikali ya kukata maposho yasiyoyalazima ili fedha hizo ziweze kusaidia katika kuendeleza majukumu na mipango ya Serikali. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Wizara hiyo kwa kuwasilisha vyema Mpango wake wa kazi na kuwataka viongozi na watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili waendelee kupata mafanikio. Pamoja na hayo, Dk. Shein alisisitiza umuhimu wa uzalendo katika utekelezaji wa majukumu na kueleza kuwa suala zima la uzalendo litapewa kipaumbele mafanikio makubwa yanaweza kupatikana. Nae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Wizara hiyo na kusisitiza haja ya kuendelezwa vuguvugu la mashindano katika skuli mbali mbali hapa nchini ili kuweza kupata wanamichezo wazuri sambamba na kuongeza vipaji vya vijana katika sekta ya michezo. Balozi Idd nae alitumia fursa hiyo kuihakikishia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuwa ataendelea kushirikiana na kuisaidia Wizara hiyo ili kuweza kupatikana elimu iliyo bora hapa nchini. Nae Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alisisitiza umuhimu wa usimamizi katika skuli hapa nchini na kuwataka walimu wakuu na wasaidizi wao kushirikiana kwa pamoja katika kulifanyia kazi suala hilo ili elimu bora iliyokusudiwa iweze kupatikana. Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma alieleza kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, Wizara yake inaendelea na malengo ya kupanua upatikanaji wa huduma za elimu na kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa. Alisema kuwa Wizara imeweka vipaumbele katika kufikia dhamira ya utoaji wa elimu bora kwa wote na kuweza kupanga mipango mbali mbali ikiwemo kuimarisha elimu ya Maandalizi, kutayarisha na kuchapisha miongozo ya walimu, kuimarisha elimu na Msingi, kuimarisha Elimu ya Sekondari, Kuimarisha Elimu Mbadala na Watu wazima na kuimarisha elimu ya juu. Aidha, Waziri Pembe alisema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu Julai hadi Septemba 2016, Wizara hiyo imeweza kutekeleza malengo mabli mbali yakiwemo matayarisho ya Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Elimu kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2021) yameanza. Pamoja na hayo, alieleza kuwa ujenzi wa vituo viwili vya Mafunzo ya Amali huko Makunduchi na Daya nao umeanza pamoja na ujenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu Mazizini umekamilika. Alieleza kuwa Wizara hiyo imepokea jumla ya madawati 5,150, Viti 1630 na meza 600, samani ambazo zimepokelewa kutoka kwa Wabunge, Wawakilishi na Diaspora. Vile vile alieleza kuwa ujenzi wa jengo jipya la Taasisi ya Utalii Maruhubi unaendelea na umefikia asilimia 20 na ujenzi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume nao unaendelea na umefikia asilimia 30 ambapo pia, ujenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Amali Wingwi Mtemani nao unaendelea na umefikia asilimia 90.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo