Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wizara ya Fedha na Mipango iko vizuri katika ukusanyaji wa mapato.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Fedha na Mipango iko vizuri katika ukusanyaji wa mapato. Dk. Shein aliyasema hayo, Ikulu mjini Zanzibar katika kikao maalum kati yake na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba katika Bajeti ya mwaka 2016-2017. Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajiweza na iko vizuri katika ukusanyaji wa mapato yake hali ambayo inatoa mwanga wa mafanikio katika kuendeleza shughuli zake za maendeleo na kukuza uchumi. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuendesha vizuri matumizi ya kawaida kwa Wizara zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuziwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi. Pamoja na hayo, Dk. Shein alipongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Taasisi za ukusanyaji wa mapato katika Wizara hiyo kwa kuendelea kukusanya mapato ipasavyo na hatimae kusaidia na kukuza uchumi wa nchi. Sambamba na hayo, Dk. Shein alisisitiza haja kwa Wizara hiyo kutenga bajeti maalum kwa ajili ya utafiti hapa Zanzibar kwani maendeleo ni utafiti. Nae Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alitoa pongezi kwa Wizara hiyo kwa kuwasilisha vyema mpango wake wa kazi katika utekelezaji wa Bajeti ya Julai hadi Septemba mwaka 2016-2017 na kusisitiza haja kuongeza juhudi katika kufanya tafiti mbali mbali ndani ya Wizara hiyo. Mapema Kaimu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Salama Aboud Talib alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango ina jukumu la kusimamia masuala ya Fedha za Umma kama ilivyoelezwa ndwani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Sura ya Saba. Alisema kuwa miongoni mwa majukumu hayo ikiwemo kukusanya rasilimali fedha za Serikali, kuzigawa rasilimali hizo kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali na kusimamia matumizi yake. Aidha, alisema kuwa Wizara inatekeleza majukumu na shughuli zake kwa kufuata miongozo na sheria mbali mbali za Wizara zinazohusu masuala ya usimamizi wa fedha na Mipango ya Kitaifa. Pamoja na hayo, uongozi huo wa Wizara ya Fedha ulitoa pongezi kwa Rais kwa kuendelea kuwapa miongozo mizuri ambayo imekuwa chachu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo