Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Serikali itandelea kuchukua hatua kali dhidi ya Wawekezaji wasio waadilifu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali imeweza kuongeza mapato yake kwa kuwa wawekezaji wa ndani na wa nje wamekuwa wakilipa kodi stahiki na kwa wakati.Hata hivyo amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wawekezaji wakwepa kodi na wasio waadifu. Akifungua Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Wawekezaji wa Sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) unaofanyika katika HOTELI ya Park Hyatt mjini Unguja leo, Dk. Shein ametoa wito kwa wawekezaji na wafanyabiashara kuzingatia misingi ya ukweli, uadilifu na uwazi katika kuendesha shughuli zao.“Inatia moyo kuona wawekezaji katika sekta ya Utalii wamekuwa wakiunga mkono jitihada za serikali za kuongeza mapato halikadhalika katika kutekeleza mpango wetu wa Utalii kwa Wote” Dk. Shein alisema. Xby Counterflix Sambamba na wito huo, Dk. Shein amewapongeza na kuwashukuru wawekezaji katika sekta hiyo na nyingine kwa michango yao kusaidia jamii ambayo inatokana na faida wanayopata kutoka biashara zao.Kwa hivyo amewahakikishia wanachama wa ZATI na washirika wengine katika sekta ya utalii kuwa serikali yake itaendelea kufanya kazi nao kwa karibu na kuwapa ushirikiano unaostahiki. Katika hotuba yake hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Rashid Ali Juma, Dk. Shein amesifu jitihada za ZATI kwa kushirikiana na Kamisheni ya Utalii katika kuitangaza Zanzibar katika masoko ya utalii kote ulimwenguni.Alibainisha kuwa matokeo ya jitihada hizo ni kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaoitembelea Zanzibar hadi kufikia watalii 311,801 mwaka 2014 ambapo lengo ni kupata watalii 500,000 ifikapo mwaka 2020. Hata hivyo, Dk. Shein alieleza kuwa jitihada za kuongeza idadi ya watalii hazina budi kwenda sambamba na hatua za kuwafanya watalii hao wawapo Zanzibar kutembelea sehemu mbalimbali za historia.“takwimu zinaonesha kuwa kuna pengo kubwa kati ya idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar na idadi ya watalii wanaotembelea sehemu zetu za kihistoria hasa kisiwani Pemba” Dk. Shein alibainisha. Alifafanua kukosa watalii kutembelea sehemu nyingi za kihistoria siyo tu kuwa Zanzibar inapoteza fursa adhimu ya kutangaza historia na utamaduni wake nje lakini pia inakosa fedha nyingi ambazo hutolewa kama viingilio kwa watalii hao katika sehemu hizo.Katika mnasaba huo, ametaka kuimarishwa kwa ushirikiano katika kuitangaza sekta ya Utalii Zanzibar na kusisitiza kuwa ni ushirikiano huo tu ukiambatana na mipango thabiti ndio itakayowezesha Zanzibar kuwa mshindani wa kweli katika masoko ya utalii duniani. Xby Counterflix Dk. Shein aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa amefurahishwa na namna ZATI ilivyojiimarisha kwa kuwaunganisha wawekezaji katika maeneo mbalimbali ya sekta ya utalii na kuifanya ZATI kuwa taasisi moja muhimu katika kuimarisha sekta ya utalii Zanzibar.Aliongeza kuwa amefurahi “kuona katika mkutano huu bodi ya ZATI imewaalika wataalamu kutoka fani mbalimbali zikiwemo za kodi, uhamiaji, kazi, miundombinu, mafuzo (training),uhifadhi, huduma za maji na umeme,mazingira na vyombo vya usalama” Akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa ZATI bwana Seif Miskry alieleza kuwa taasisi yake itaendelea kufanya kazi kwa pamoja na serikali na taasisi zake ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inatoa matokea yanayotarajiwa. Alibainisha kuwa sekta hiyo imekuwa ikikuwa mwaka hadi mwaka lakini kumekuwepo na changamoto nyingi ambazo zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa ushirikiano wa washirika wote katika sekta hiyo. Moja ya changamoto hizo sekta hizo Mwenyekiti huyo aliitaja kuwa ni suala la kodi nyingi wanazotozwa wawekezaji katika sekta hiyo ambapo pamoja na kuwa ZATI imekuwa ikifanya mashauriano ya mara kwa mara na serikali lakini bado suala hilo halijafikia mahala pazuri.Kwa kivyo alitoa wito kwa Mheshimiwa Rais kulichukua suala hilo kama alivyolishughulikia suala la ulinzi na usalama wa watalii ambapo alikutana na washirika muhimu wa sekta hiyo kulijadili na kulitafutia ufumbuzi. Xby Counterflix “Tulikuwa na changamoto ya usalama wa watalii, Mheshimiwa Rais alichukua jitihada binafsi kulishughulikia na hili la kodi ni vyema akafanya hivyo hivyo” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa sera ya kodi ni muhimu kwa serikali na zaidi kwa ustawi wa sekta hiyo. Bwana Miskry alihimiza mchango zaidi wa serikali katika kutangaza utalii kwani kwa sasa inaonekana kazi hiyo inafaywa zaidi na wawekezaji zaidi wenyewe.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo