Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Balozi Seif Akutana na Rais wa Makampuni ya Kimataifa ya Vitega Uchumi.
Kasi kubwa ya uchumi wa Tanzania inayoonekana kupanda kwa haraka katika kipindi kifupi imeanza kutoa ushawishi mkubwa kwa Makampuni na Taasisi za Kimataifa kuonyesha dalili za kutaka kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi na maendeleo ili kuunga mkono kasi hiyo. Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Sita wa Kampuni hiyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Bara ara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam. Bwana Koichi Kawaji alisema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na Wataalamu wa masuala ya Uchumi Duniani umebaini kwamba kasi ya uchumi wa Taifa la Tanzania unaongoza ikilinganishwa na Mataifa yaliyomo ndani ya Bara la Afrika kwa hivi sasa . Kiongozi huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Koto alifahamisha kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika yenye muelekeo mpana wa Uchumi wake kukuwa kwa haraka ukifananishwa na Nchi ya Singapore Bwana Koichi alisema wataalamu wa Kampuni ya Koyo wamelazimika kufanya ziara ya makusudi katika azma ya kujionea kasi hiyo Nchini Tanzania na kuangalia maeneo ambayo Taasisi hiyo ya Uwekezaji inaweza kutumia fursa zilizopo katika kusaidia ukuaji wa Uchumi wa Tanzania. Alieleza kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilmali za kutosha za Kiuchumi ambazo kwa namna nyingi Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchini wanaweza kutumiwa vyema katika njia ya kuingia ubia na Serikali, Makampuni au hata Watu binafsi wenye sifa na shauku ya kuwekeza. Rais huyo wa Kamuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi alielezea furaha yake kutokana na utulivu mkubwa na Amani iliyotanda Nchini Tanzania katika kipindi kirefu sasa. Alisema amani na utulivu huo kwa kiasi kikubwa ndio iliyozaa mafanikio makubwa ya Uchumi yanayoendelea kupatikana na hatimae kuchangia mapato ya Taifa sambamba na kupunguza umasikini lakini kwa njia nyengine pia umezuia mfumko wa bei unaotoa afueni ya maisha bora kwa Wananchi walio wengi. Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishauri Serikali ya Japani kupitia ujumbe wa Kampuni hiyo ya Koyo kuangalia maeneo ambayo Taasisi na Makamuni ya Nchi hiyo yanaweka kuwekeza. Balozi Seif alisema Tanzania imepakana na Bahari kuu eneo ambalo Japan kutokana na kuendelea Kiviwanda inaweza kusaidia Taa luma katika Mpango wa kulielekeza Taifa la Tanzania kuwa Nchi ya Viwanda ifikapo Mwaka 2025. Alisema Tanzania bado ina fursa nzuri ya kujifunza Taaluma ya Uvuvi wa Bahari kuu kwa kuanzishwa Viwanda vya usindikaji bidhaa zinazotoka na mazao ya Baharini kama Samaki wa aina mbali mbali pamoja na zao laMwani. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibat itakuwa tayari kutoa msaada wowote utakaohitajiwa na Kampuni hiyo wakati itakapofikia hatua ya kutaka kuwekeza miradi yake Visiwani Zanzibar.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo