Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Serikali yasitisha utoaji wa Mikopo ya Elimu ya juu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamisha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu hadi hapo serikali itakapojiridhisha na utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo hiyo.“Hatutatoa mikopo mwaka huu mpaka hapo tutakapokamilisha kazi ambayo tumeanza kuifanya ya kupitia upya utaratibu wa utoaji mikopo hiyo ili kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa kulingana na mahitaji ya sasa ya nchi na kwa wanaostahiki” alieleza Dk. Shein Serikali yasitisha utoaji wa Mikopo ya Elimu ya juu. Akizungumza katika hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofaulu daraja la kwanza katika Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne mwaka 2015 na Kidato cha Sita mwaka 2016, Dk. Shein ameeleza kuwa katika utaratibu wa sasa wapo waliodanganya kupata mikopo na ambao wamekopeshwa lakini wamekuwa wagumu kurejesha mikopo hiyo.Katika halfa hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Issa Haji Usii Gavu, jumla ya wanafunzi 119 waliomaliza kidato cha nne na wengine 50 waliomaliza kidato cha sita walipewa zawadi kwa kupata daraja la kwanza katika mitihani yao ya taifa. Xby Counterflix “Wako waliokejeli matokeo yenu lakini ukweli ni huo muko 50 wa kidato cha tano mliopata daraja la kwanza na wengine 119 mliofaulu daraja la kwanza mtihani wa kidato cha nne” alieleza Dk. Shein na kuhoji msingi wa kukebehi matokeo hayo.Aliongeza kuwa ufaulu wa wanafunzi hao ni sifa kwa Zanzibar na anaamini kwa hatua zinazochukuliwa na serikali kuimarisha miundombinu ya elimu pamoja rasilimali watu kiwango cha ufaulu kitazidi kuongezeka. “mnapofanya mitihani sote tunakuwa na wasi wasi; nyinyi wenyewe, walimu, wazazi na sisi serikali kwa kuwa tunaelewa kuwa matokeo yeyote yale ni yetu sote kama ni mazuri ni furaha yetu sote na kama si mazuri ni huzuni yetu sote” Dk. Shein aliwaambia wanafunzi hao.Dk. Shein aliwataka wanafunzi hao kujivunia fursa waliyoipata na kuitumia vyema kujiimarisha kielimu kwa kuwa haikuwa rahisi kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 kuona vijana kutoka familia masikini wanapata fursa za kuingia sekondari kwa makundi. “Mmepata bahati kubwa serikali yenu imeweka mazingira mazuri ya kupata elimu na haya ni matokeo ya utekelezaji wa ahadi ya Chama cha Afro-Shirazi na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume ya kutoa elimu bure itakaposhika madaraka” Dk. Shein alieleza.Katika hatua nyingine Dk. Shein ametoa wito kwa walimu wakuu kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri walimu katika skuli zao pamoja na kuwahimiza wakaguzi wa skuli kutimiza wajibu wao ipasavyo. Dk. Shein alibainisha kuwa kumekuwepo na tatizo la usimamizi maskulini hivyo Serikali “itatengeneza utaratibu wa kuwapatia motisha walimu wakuu na wakaguzi watakaofanya vizuri kwa kuwa ni dhahiri kuwa walimu wakuu wakisimamia vyema skuli zao na wakaguzi wakaifanya kazi yao ya ukaguzi kwa umakini tutapata matokeo mazuri zaidi” Xby Counterflix Katika salamu zake hizo kwa wanafunzi hao ambao walisindikizwa na uongozi wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, pamoja na walimu wakuu wa baadhi ya skuli, Dk. Shein aliwataka walimu kuongeza ari ya kufundisha na kwamba ni heshima na furaha ya mwalimu kuona mwanafunzi wake anapata matokeo mazuri.“wakati wetu walimu waliwapenda na kuwajali sana wanafunzi wao. Walijivunia wanafunzi wao na wanafunzi walijivunia walimu wao katika hali kama hiyo matokeo yeyote ya mtihani yaliwagusa hisia za wote; walimu na wanafunzi” Dk. Shein alieleza. Kuhusu changamoto ambazo wanafunzi hao walizieleza katika risala yao, Dk. Shein aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa zinazifanyia kazi ambapo alibanisha kuwa serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia itajenga skuli nyingine za sekondari 10 za ghorofa Unguja na Pemba ili kuimarisha miundombinu ya elimu pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya kuimarisha maabara pamoja na ununuzi wa samani ikiwemo vikalio kwa wanafunzi. Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzio ya Amali Mheshimiwa Riziki Pembe Juma alimhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa Wizara yake imejidhatiti kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inazidi kupata mafanikio pamoja na kuwepo changamoto kadhaa ambazo aliishukuru serikali kwa jitihada zake zakuzitafutia ufumbuzi.Katika risala yao, wanafunzi hao waliahidi kuongeza juhudi katika masomo yao ili safari yao ya kutafuta elimu iwafikishe katika viwango vya juu vya elimu. Walimpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuwapatia waziri mwanamke ambaye ametokea kwenye fani ya ualimu hivyo kuzielewa vyema changamoto zinazowakabili walimu na sekta nzima ya elimu.Katika risala hiyo walitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kuwa ni pamoja na uhaba wa walimu wa sayansi, maabara zenye viwango bora na upungufu wa vikalio. Xby Counterflix Akitoa salamu za shukrani kwa mgeni rasmi Mwalimu Arabia Awadh Salum alisema tukio hilo la kukutana na Mheshimkiwa Rais litasaidia kuongeza hamasa kwa watoto kufanya vizuri na kuahidi kuongeza juhudi ili wanafunzi wafikie viwango bora vya ufaulu vilivyowekwa.Aliongeza kuwa ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sita kwa Zanzibar si chini ya wastani wa asilimia 70.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo