Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Mhe:Dk.Shein ataka taratibu za kufanya Tafiti Zanzibar kurahishiwa kuepuka Urasimu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK Ali Mohamed Shein ameitaka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kukaa pamoja na Tume ya Mipango na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kuangalia utaratibu bora zaidi wa kuratibu shughuli za utafiti hasa baada ya Zanzibar kuwa na mpango wake wa utafiti ambao umeainisha maeneo yake ya utafiti na vipaumbele vyake.Akizungumza katika kikao cha kupita taarifa ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichofanyikia,Dk. Shein alieleza kuwa katika mazingira ya sasa ambapo Zanzibar imeainisha ajenda zake za utafiti kuna haja ya kuhakikisha kuwa taratibu za kufanya utafiti Zanzibar zinarahishwa ili kuepuka urasimu. “Nadhani utaratibu uliopo sasa ni wa zamani, turahishishe taratibu zetu. Tuzingatie mazingira ya sasa ambapo tuna wanafunzi wengi, wakufunzi na watafiti wengi lakini zaidi tuna ajenda zetu za utafiti ambazo tunataka kuzitekeleza” Dk. Shein alieleza.Katika kikao hicho Dk. Shein alieleza kuwa utaratibu wa bangokitita ni mkakati makini wa kuimarisha utendaji serikalini ambao unazingatia utendaji na uwajibikaji wa pamoja. Aliongeza kuwa kwa sasa wizara nyingi zimeonesha mabadiliko makubwa katika utendaji wao na kwamba vikao vya kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za serikali zinaonesha mabadiliko hayo.Alieleza kuwa hivi sasa watendaji wengi serikalini wanajituma na kuonesha umakini katika kazi zao kutokana na mfumo huu ambao unaweka bayana majukumu na mgawanyo wa fedha katika shughuli ya serikali kwa kila kipindi. “Bangokitita ni zaidi ya baadhi ya watu wanavyoelewa. Ni utaratibu ambao unatupa fursa ya kuuliza maswali na kutafuta majibu yake kwa pamoja na unajenga ari ya kufanya vizuri zaidi na kumuongezea kila mtendaji uelewa wa majukumu ya wizara nzima” Dk. Shein alieleza.Katika kikao hicho Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi aliwashukuru viongozi na watendaji wa Ofisi yake kwa kufanya kazi kwa bidii na kueleza kuwa maswali yaliyoulizwa katika kikao hicho yanatoa fursa kwao kujisahihisha na hivyo kufanya vizuri zaidi katika utekelezaji majukumu yao. Aidha alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa miongozo mbali mbali anayotoa katika vikao hivyo ambayo imekuwa chachu katika kuimarisha utendaji serikalini. Akizungumza kabla ya kuwasilisha Taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed alieleza kuwa katika kipindi hicho Ofisi yale imetekeleza shughuli mbalimbali ambazo zimezingatia mipango mbali ya maendeleo, Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na Maelekezo ya Hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoyatoa katika hotuba yake ya ufunguzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi. Aidha alibainisha kuwa katika robo hiyo ya kwanza wizara hiyo pamoja na taasisi zake ilipatiwa jumla ya shilingi bilioni 10.2 ikiwa ni asilimia 101 ya bajeti ya wizara hiyo ya shilingi bilioni 10.1 kwa kipindi hicho.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo