Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Serikali kuhakikisha fedha zilizoahidiwa kwenye bajeti zinapatikana
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezihakikishia Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa juhudi zitaendelea kuchukuliwa katika upatikanaji wa fedha kwenye vifungu vya matumizi ya Bajeti za Wizara hizo ili zifanye kazi kwa ufanisi zaidi. Dk. Shein aliyasema ha yo leo Ikulu mjini Zanzibar katika kikao maalum kati yake na uongozi wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ilipowasilisha Taarifa yake ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba katika Bajeti ya mwaka 2016-2017. Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa hatua kubwa imefikiwa katika upatikanaji wa fedha kwa kila Wizara katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na mikakati maalum iliyowekwa ambayo hatimae imeleta mafanikio makubwa. Dk. Shein alisema kuwa juhudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuondoa matumizi yasio ya lazima yakiwemo maposho, safari na mambo mengineyo zimesaidia kwa kiasi kikubwa na ndio maana lengo litafikiwa la kuwaongezea hata mishahara wafanyakazi wa sekta ya umma. Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi na watendaji wote wa Wizara hiyo kwa kuwasilisha vyema Mpango Kazi wao. Mapema Kaimu Waziri wa Wizara hiyo, Issa Haji Ussi Gavu akisoma taarifa ya Mapango Kazi huo alisema kuwa jukumu la msingi la Ofisi hiyo ni kusimamia masuala yanayohusu utawala wa sheria na utumishi wa umma pamoja na kuimarisha upatikanaji bwa haki. Aidha, Waziri Gavu alisema kuwa Ofisi ina jukumu la kusimamia na kuratibu utekelezaji wa misingi ya utawala bora katika taasisi za umma. Kaimu Waziri huyo, alisoma malengo ya Wizara hiyo, pamoja na madhumuni ya taarifa, utekelezaji kifedha ambapo miongoni mwa malengo ya Wizara hiyo ni kusimamia utoaji na upatikanaji wa haki, kukagua hesabu za serikali, kuwajengea uwezo watumishi wa umma, kusimamia mali za Wakfu, kukusanya Zaka, Sadaka na Misaada ya kheri na kuigawa kwa wanaostahiki pamoja na malengo mengineyo. Mapema Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee nae alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Wizara hiyo kwa uwasilishaji mzuri wa Mpango Kazi wake. Katika maelezo yake Dk. Mzee alisema kuwa licha ya ukubwa wa Wizara hiyo lakini imeuweka vizuri mpangilio na uwasilishwaji wa kazi hiyo huku akitoa wito kwa Wizara hiyo kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi kwa kutambua kuwa Wizara hiyo ni kioo kwa Wizara nyengine za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nao uongozi wa Wizara hiyo, ulitoa pongezi za pekee kwa Dk. Shein kwa kupatiwa fedha za kutosha katika vifungu vya matumizi kwenye Bajeti yao pamoja na Bajeti za Wizara zote za Serikali hatua ambayo imezidi kuwapa ari katika kutekeleza majukumu yao ya kazi. Uongozi huo ulimuhakikishia Dk. Shein kuwa haotomuangusha na umeahidi kutekeleza vyema majukumu yao na kusisitiza kuwa utaendelea kuchapa kazi ili kufikia malengo yaliokusudiwa. Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Asha Ali Abdulla alitumia fursa hiyo kusoma taarifa ya utekelezaji wa mpango Kazi kwa robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba mwaka 2016 pamoja na muhtasari wa upatikanaji wa fedha kwa kipindi hicho kwa Taasisi zote za Wizara hiyo. Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo