Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Viongozi jiepusheni na vitendo vinavyokiuka maadili ya Viongozi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewakumbusha viongozi kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili ya viongozi na kujiepusha na mambo yanayokwenda kinyume na maadili hayo Dk. Shein amesema hayo jana wakati akihitimisha kikao cha kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ambacho kilihusisha viongozi na watendaji waandamizi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Aliwatahadharisha viongozi na watendaji hao kuwa wakati watakapotakiwa kujaza fomu za maadili wahakikishe kuwa wanatoa taarifa za kweli kwa kuwa jambo hilo ni zito na kwamba Tume ya Maadili itafuatilia kwa makini taarifa hizo.Katika kikao hicho, Dk. Shein aliwataka viongozi na watendaji hao kuzingatia sheria na Katiba wakati wote wa kutekeleza majukumu yao ili kuepusha malalamiko ya uvunjaji wa sheria na haki za binadamu. “Katika kufanyakazi lazima muangalie sheria na Katiba. Kama kiongozi ana wasiwasi na sheria amuulize mwanasheria wa Ofisi yake na kama hakuridhika hana budi kupata ushauri kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu” Dk. Shein alisisitiza.Katika kikao hicho ambacho kwa mara ya kwanza kila Mkuu wa Mkoa katika mikoa mitano ya Zanzibar aliwasilisha taarifa ya utekelezaji kazi katika mkoa wake, Dk. Shein alirejea wito wake wa kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuwa karibu na wananchi ili kufahamu kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. “Shughuli za Wizara zote 13 ziko huko (Mikoani na Wilayani) kwa hivyo lazima mufike huko mfuatulie na wananchi wawaone kuwa mnahangaika kuwatumikia sio kukaa maofisini” alisisitiza Dk. Shein na kuongeza kuwa wizara hiyo ikifanya vizuri maana yake serikali imefanikiwa.Katika mnasaba huo, Dk. Shein amezitaka Halmashauri na Mabaraza ya Manispaa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kusisitiza kuwa fedha zinazokusanywa lazima zitumike katika shughuli za wananchi badala ya kutumia zaidi katika masuala ya utawala. “Tunataka fedha zinazokusanywa matumizi yake yaelekezwe zaidi kwenye kushughulikia matatizo na kuimarisha huduma kwa wananchi sio matumizi mengine ambayo hayana mnasaba na ustawi wa wananchi” Dk. Shein alieleza.Kwa hivyo alipongeza hatua za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wa kupambana na kero za wananchi kama vile magereji maeneo ya makazi ya watu, tatizo la utupaji ovyo wa takataka, tatizo la ombaomba, kuzagaa ovyo kwa mifugo mjini, uchumbaji ovyo wa mchanga na upigaji ovyo wa muziki maeneo ya makazi. Aidha, aliwataka viongozi na watendaji hao kufanya tathmini ya majadiliano ya kikao hicho ili kila mmoja atakaporejea ofisi kwake ajue namna ya kujipanga kutekeleza majukumu kwa ufanisi zaidi. Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushughulikia matatizo katika maeneo yao pasi na kuyapa nafasi matatizo hayo kufikishwa kwa viongozi wakuu wa Serikali.Alisema wakuu wa mikoa na wilaya hawana budi kuwaelimisha wananchi kufika katika ofisi zao wanapokuwa na matatizo badala ya matatizo hayo kufikishwa kwa viongozi wa kitaifa bila ya kupitishwa katika ofisi zao. “Wananchi wengi wanafika kwetu kuleta matatizo yao. Jitahidini kuyatatua huko huko nyinyi wenyewe ama yakifika kwetu yawe nyinyi yamewashinda” aliwaambia viongozi hao na kuwataka wajiepueshe kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi. Kwa upande wake Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa Haji Omar Kheri alieleza kuwa Sheria ya Mamlaka ya Tawala za Mikoa Nam. 8 ya mwaka 2014 na Sheria ya Serikali za Mitaa Nam. 7 ya mwaka 2014 imeziondoa mamlaka hizo kutoka shughuli za uratibu tu hadi kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo katika mikoa.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo