Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Ndoto yetu ni kuwa na huduma bora kwa Watoto na Kinamama katika Hospitali ya Mnazi Mmoja imetimia
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein ameuhakikishia ujumbe kutoka Chuo Kikuu Cha Haukeland cha nchini Norway kuwa daima atakuwa msatri wa mbele kuunga mkono ushirikiano kati ya chuo hicho na hospitali ya Mnazi Mmoja. Akizungumza na ujumbe huo ambao uliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa chuo hicho bwana Eivind Hansen, Dk. Shein alisema ushirikiano kati ya chuo hicho na hospitali hiyo umechangia sana katika kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya Zanzibar.Aliuambia ujumbe huo ambao umewasili Zanzibar leo kuhudhuria uzinduzi wa Wodi ya Watoto na Wodi ya Wazazi katika hospitali ya Mnazi Mmoja utakaofanyika kesho kuwa ndoto yake ya kuwa na huduma afya bora na za kisasa kwa watoto Zanzibar imetimia. Ni ushirikiano ambao umeleta faraja kwa wananchi wetu na watoto wetu kutokana na kuimarika huduma za afya zinazotolewa wa watoto wetu” Dk. Shein alieleza kwa furaha.Dk. Shein aliuambia ujumbe huo ambao ulimjumuisha Bwana Trond Mohl ambaye ni mfadhili mkuu wa ujenzi wa jengo hilo kuwa wananchi wa Zanzibar wanathamini sana mchango huo. Alisema milango iko wazi kwa Chuo hicho kuimarisha ushirikiano wake katika sekta ya afya na kueleza furaha yake kwa taarifa kuwa baada ya kukamilika mradi huo chuo hicho sasa kiko katika mazungumzo kusaidia kuimarisha hospitali ya wagonjwa wa akili ya Kidongo Chenkundu.“sina budi kutoa shukrani zangu za moyoni kwa habari hii ya Chuo Cha Hukeland kusaidia kuimarisha huduma za wagonjwa wa akili na kuimarisha majengo ya katika hospitali ya Kidongo Chekundu” Dk. Shein alisema. Dk. Shein alimshukuru Bwana Trond Mohn kwa kuonesha dhamira ya kusaidia hospitali hiyo ya Kidongo Chekundu na kueleza uamuzi huo umekuja wakati muafaka kutokana na magonjwa ya akili kuwa ni moja ya changamoto zinazikabili sekta ya afya nchini.Dk.Shein alitumia fursa hiyo kueleza na kupongeza uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Norway na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ikiwemo na kubainisha kuwa ushirikiano wa taasisi hizo mbili ni mfano wa matunda ya uhusiano huo. Akizungumza katika mkutano huo Mfisa Mtendaji wa chuo hicho Bwana Jonsen kazi imekuwa rahisi hapa Zanzibar kutokana ushirkiano mzuri ambao timu yake imekuwa ikipata kutoka viongozi wa wizara ya Afya na hospitali ya Manzi Mmoja.Alibainisha kuwa chini ya ushirikiano huo pande mbili hizo zimekuwa zikibadilishana wataalamu ambapo hadi sasa wataalamu wa afya 30 kutoka Zanzibar wamapata fursa za kujifunza nchini Norway na wataalamu 20 wa nchi hiyo wamefika Zanzibar. “Tunataka ushirikiano huu uwe thabiti zaidi kwa kubadilishana uzoefu na kuongeza uwezo wetu pande zote ili tuweze kutoa huduma bora zaidi na za mfano” alisema Bwana Hansen.Bwana Hasen alisema chuo chake kitaendelea kushirikiana na hospitali ya Mnazi Mmoja kuongeza kuwa “baada ya kukamilisha jengo la watoto sasa tunataka kusaidia hospitali ya wagonjwa wa akili” alimazlizia. Mkutano huo ulihudhuria pia na viongozi wa wizara ya afya wakiongozwa na Waziri wake Mheshimiwa Mahmod Thabit Kombo.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo