Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Ufanisi katika utendaji wa kazi ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano mwema kati ya viongozi.
KATIBU Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee ameeleza kuwa njia pekee ya kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano mwema kati ya viongozi na watendaji wao. Dk. Mzee alisema kuwa mahusiano na mashirikiano yanapopewa kipaumbele miongoni mwa viongozi wenyewe ama kati ya viongozi na watendaji wao katika sehemu yoyote ya kazi ufanisi wa kazi huwa mkubwa. Maelezo hayo ameyatoa leo wakati alipokutana na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi huko katika ukumbi wa Baraza la Mapinduzi, Forodhani mjini Zanzibar. Katika maelezo yake, Dk. Abdulhamid aliueleza uongozi huo umuhimu wa kuendeleza uhusiano na ushirikiano mwema miongoni mwao pamoja na watendaji wao kwa lengo la kuleta ufanisi kazini sambamba na kufikia azma ya kuiletea nchi maendeleo endelevu. Aidha, aliwataka Wakuu wa Idara kusimamia suala zima la nidhamu na uwajibikaji katika taasisi zao hasa ikizingatiwa kuwa suala zima la utoro na uchelewaji kazini bado ni tatizo ambalo linazorotesha utendaji wa kazi na utoaji huduma bora kwa wananchi. Hivyo, aliwataka viongozi hao kutambua kuwa wao ni dhamana na wanawajibika kwa wale wote wanaowaongoza ambapo pia, wanapaswa kuwa mfano wa kuwahi kazini, kukaa maofisini na kufanya kazi zao ipasavyo. Aidha, Dk. Mzee, aliwaeleza viongozi hao kuwa mbali ya majukumu yao mengine ya kazi ni vyema wakaelewa kuwa wana jukumu kubwa la kumsaidia Rais ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake kwa wananchi na kuwaletea maendeleo wanayohitaji. Pamoja na hayo, aliueleza uongozi huo kuwa wana wajibu wa kuyatangaza mafanikio makubwa yaliopatikana katika taasisi zao ili wananchi watambue juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali yao pamoja na viongozi wao chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein. Dk. Mzee alisisitiza haja kwa Wakuu wa Idara kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi hasa ikizingatiwa kuwa kila mmoja ameteuliwa kwa kuzingatia uzoefu na utaalamu alionao. Dk. Mzee, aliwataka Wakuu wa Idara zote za Serikali, kuelewa kuwa jukumu la kutekeleza na kusimamia mipango yote ya Idara zao kwa Unguja na Pemba wanalo wao huku wakitambua kuwa Afisa Mdhamini kazi yake kubwa ni kuratibu shughuli zote za Pemba hivyo, wanapaswa kupanga, kufuatialia na kuzitambua shughuli zote za Idara zao kwa upande wa Pemba. Pamoja na hayo, Dk. Mzee aliupongeza uongozi wa Ofisi hiyo kwa kuendeleza ushirikiano miongoni mwao pamoja na watendaji wao ambapo aliwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi huku wakitambua kuwa kwa mujibu wa ofisi yao wao wawe kigezo cha ufanisi kwa ofisi nyengine. Sambamba na hayo, Dk. Mzee alitumia fursa hiyo kuendelea kutoa miongozo na taratibu za utayarishaji wa Taarifa za Utekelezaji wa Mpango Kazi wa mwaka na robo mwaka wa Bajeti za Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nao viongozi mbali mbali wa Taasisi ya Ofisi hiyo, walieleza kufarajika kwao na maelekezo na mwongozo walioupata katika mkutano huo kutoka kwa Kiongozi huyo na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliozungumzwa huku wakimpongeza kwa uzoefu na weledi wake wa muda mrefu ambao umekuwa chachu katika utendaji wao wa kazi.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo