Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Uzinduzi wa Hospitali mpya ya Abdalaa Mzee kumeandika histroai ya utoaji huduma za afya Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema uzinduzi wa hospitali mpya na ya kisasa ya Abdalla Mzee kumeandika historia mpya katika utoaji wa huduma za afya kisiwani Pemba.Amesema kuzinduliwa kwa hospitali hiyo kunaifanya Zanzibar kuwa na hospitali mbili kubwa zinazolingana kiuwezo huku hatua zikiendelea kuchukuliwa kuimarisha hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa. Uzinduzi wa Hospitali mpya ya Abdalaa Mzee kumeandika histroai ya utoaji huduma za afya Pemba Katika hotuba yake akizindua hospitali hiyo iliyoko Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba leo, Dk. Shein alieleza kuwa hospitali hiyo imefikia kiwango cha hospitali ya Mkoa kutokana na miundombinu yake, vifaa na wataalamu.Aliwaeleza viongozi, wageni waalikwa wakiwemo mabalozi na maelfu ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo kuwa hospitali hiyo ina vifaa vyote muhimu vya kisasa vya uchunguzi pamoja na huduma na mifumo ya uchunguzi wa magonjwa ambayo haipatikani katika katika baadhi ya hospitali kubwa nchini. Alifafanua kuwa hospitali hiyo iliyogahrimu shilingi bilioni 35 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya Watu wa China kuwa kutokana na bora wake haitashangaza watu kutoka nje ya kisiwa cha Pemba kufika huko kufuata matibabu.Katika hatua nyingine, Dk. Shein amesisitiza kuwa sera ya afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kutoa matibabu bure kwa kila mwananchi na kwamba hata pale wananchi wanapotakiwa kuchangia kutokana na upungufu wa baadhi ya nyenzo unaojitokeza baadhi ya wakati bado si lengo la serikali kufanya hivyo. Katika hotuba yake hiyo, Dk. Shein aliishukuru serikali na wananchi wa Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada yao kwa Zanzibar na kueleza kuwa miongoni mwa marafiki wa Zanzibar, nchi hiyo ni rafiki wake wa kweli.Aidha alipongeza kampuni ya ujenzi ya Jiangsu Provincial Construction Group kutoka China kwa kutekekeleza mradi huo kwa kipindi cha miezi 18 kama ilivyopangwa. Dk.Shein alitoa shukrani pia kwa mabalozi wa China na mabalozi wadogo wa nchi hiyo wa sasa na watangulizi wao kwa kufuatilia kwa makini ujenzi wa hospitali hiyo hadi kukamilika. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwashukuru pia wananchi waliokubali kuhama pamoja na waumini waliokubali kuhamisha msikiti kuwezesha upanuzi wa hospitali hiyo. Aliwataja pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Mohamed Saleh Jidawi na Katibu Mkuu wa Wziara ya Fedha kwa kuchagia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo.Katika maelezo yake kumkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alisema ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na wodi za watoto na wazazi katika hospitali ya Mnazi Mmoja ambazo zilifunguliwa hivi karibuni zitabaki kuwa miongoni mwa kumbukumbu nzuri za mafanikio ya uongozi wa Awamu ya Saba. Akitoa maelezo kwa mgeni rasmi na wananchi waliohudhuria sherehe hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Juma Malik Akil alieleza huduma katika hospitali hiyo kubwa na ya kisasa kisiwani Pemba itaongezeka kadri watalaamu wanaohitajika watakavyoongezeka na kupata uzoefu wa kutumia vifaa. Alibainisha kuwa hivi sasa tayari watumishi 56 kutoka Unguja wamehamishiwa katika hospitali hiyo na mipango iko mbioni kuongeza watumishi zaidi.Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa kukamilika kwa hospitali hiyo kutatoa fursa zaidi kwa wanafunzi wanaochukua mafunzo katika fani mbali mbali za udaktari kufanya mazoezi katika hospitali hiyo. Akizungumza katika sherehe hizo Balozi wa China nchini Mheshimiwa Dk. Lu You Quin alisema nchi yake inathamini sana ushirikiano wake na Zanzibar na kueleza kuwa miradi mingi ya maendeleo ambayo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana kwa miaka zaidi ya 50 sasa ni kielelezo cha urafiki huo. Alimhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali na wananchi wa Zanzibar katika kuendesha miradi zaidi iliyopo sasa itakayobuniwa baadae.Kuhusu hospitali hiyo balozi Lu You Quin alieleza kuwa madaktari na wataalamu kutoka China wataendelea kuwepo katika hospitali hiyo kusaidia uendeshaji wake kwa kutoka huduma kwa wagonjwa na pia mafunzo kwa madaktari na watumishi wa hospitali hiyo ili kudumu utoaji hudumu kwa vifaa vipya vilivyowekwa.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo