Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongezwa kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amezipongeza juhudi zinazochukuliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo. Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongezwa kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar Dk. Shein aliyasema hayo, Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na aliyekuwa Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dk. Tonia Kandiero, aliyefika Ikulu kwa ajili ya kumuaga baada ya kupewa majukumu mengine ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya (AfDB) Kuisini mwa Afrika.Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake binafsi kwa kiongozi huyo pamoja na Benki ya (AfDB) kwa namna inavyotoa ushirikiano wake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo hapa nchini. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alieleza kuwa Benki ya (AfDB) imekuwa ikichukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha miradi mbali mbali ya maendeleo hapa Zanzibar inaimarika na kuendelea kuwasaidia wananchi wote wa Unguja na Pemba.Alisema kuwa (AfBD) siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Zanzibar inapata mafanikio katika kuendeleza miradi yake mbali mbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo, Dk. Shein alizipongeza juhudi hizo ambazo zimekuwa chachu katika maendeleo ya Zanzibar. Kwa upande wa uimarishaji wa sekta ya maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefaidika kwa kupata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo ambao utasaidia katika kutatua changamoto ya uhaba wa maji katika Mkoa huo na si muda mrefu changamoto hiyo itakuwa historia.Alieleza kuwa uhaba wa maji umekuwa ni changamoto kwa baadhi ya wakaazi wa mji wa Zanzibar kwani hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu hapa nchini sambamba na tatizo la tabianchi ambalo linapelekea maji kupungua kwa kiasi kikubwa katika vyanzo vyake. Pamoja na hayo,Dk. Shein alipongeza hatua za Benki hiyo katika kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta ya Mawasiliano ya barabara kwa Unguja na Pemba ambazo zipo zilikuwa zimemalizika pamoja na zile ambazo zinatarajiwa ujenzi wake kuanza na nyengine kuendelezwa.Alieleza kuwa miradi ya barabara kisiwani Pemba itasaidia katika kuendeleza sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya utalii sambamba na juhudi nyengine zinazoendelelea kuchukuliwa na serikali kisiwani humo ikiwemo uimarishaji wa uwanja wa ndege ambayo nayo itachangia kukua kwa sekta hiyo ya utalii kisiwani humo. Aidha, Dk. Shein alisema kuwa mbali ya Benki hiyo kutoa ushirikiano wake katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo hapa nchini zikiwemo maji,barabara, kilimo, nishati, afya, elimu na utawala bora pia, imeweza kutoa mashirikiano katika nyanja nyengine za kijamii, kiuchumi na kimaendeleo. Nae aliyekuwa Mwakilishi Mkaazi huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dk. Tonia Kandiero alimueleza Dk. Shein kuwa Benki yake itaendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua na kuthamini juhudi inazozichukua katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.Dk. Kandiero alipongeza na kusifu mashirkiano mazuri yaliopo kati ya Benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein na kueleza kuwa hatua hiyo imesaidia sana katika kuleta maendeleo zaidi hapa Zanzibar. Kiongozi huyo alimuhakikishia Dk. Shein kuwa miradi yote inayosimamiwa na Benki hiyo itakamishwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara zikiwemo barabara ya Mahonda -Mkokotoni yenye urefu wa km 31, Fuoni -Kombeni km 8.6, Pale- Kiongele km 4.6 na Matemwe -Muyuni yenye urefu wa km 7.6.Pamoja na hayo, Dk. Kandiero ambaye amefanya kazi zake hapa Tanzania kwa takriban miaka sita,alimueleza Dk. Shein kuwa (AfDB) itaimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa pongezi za pekee kwa Dk. Shein na serikali anayoiongoza kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo