Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Rais wa Zanzibar Dk Shein Azindua Skuli ya Sekondari ya Kwarara Zanzibar Shamrashamra za Kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefungua skuli ya Sekondari ya Kwarara pamoja na kituo cha habari katika skuli hiyo huku akitoa wito kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuangalia ni kwa namna gani skuli hiyo itakuwa chachu ya kuwapata wanahabari. Dk. Shein alisema kuwa ipo haja kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuangalia namna namna gani skuli hiyo watatoa wanahabari kwa kutumia uwezo wa Wizara ya Elimu kupitia kituo hicho. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwaelza wananchi kuwa elimu ni jambo la mwanzo katika maisha ya mwanaadamu duniani tokea mwanaadamu alipoumbwa na haina mbadala kutokana na umuhimu wake na ndio maana juhudi za makusudi zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kwa mashirikiano ya wadau wengine. Alisema kuwa Zanzibar ilivyo leo sivyo ilivyokuwa katika miaka baada ya uhuru ambapo hadi mwishoni mwa mwezi Disemba 2016 idadi ya skuli katika ngazi ya elimu ya lazima yaani kuanzia maandalizi hadi kidatu cha nne kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 2006, imefika skuli 843 zenye wanafunzi 424,074. Aidha, alisema kuwa mwaka 1963 kabla ya Mapinduzi, wakiloni waliacha skuli mbili tu za maandalizi, skuli za msingi 62 tu na skuli za sekondari 4 pekee bila ya chuo kikuu hata kimoja. Alisema kuwa watu wa Zanzibar wanapendwa sana duniani na ndio maana wamekuwa wakiungwa mkono na ujenzi wa skuli hiyo umedhihirisha ukweli huo na kuyapongeza mashirika ya Korea likiwemo Shirika la misaada ya Kimataifa la Korea (KOICA), Good Neighbour, Seoul Broadcasting Cooperation (SBS) na Kampuni ya DONGKUK. Pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi za pekee kwa Bi Shantufe Ali Mzee ambaye ndie aliyefanya mazungumzo ya awali na baadae lakaiunganishia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na viongozi wa Shirika la Good Neighbors wakati alipokuwemo nchini Korea akifanya Shahada ya Uzamili. Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwanasihi wanafunzi wasome kwa bidii na wasihadaike na mambo mengine kwani bado kuna changamoto baadhi ya watoto kukatishwa masomo kwa ndioa au kupewa ujauzito. Kwa mujibu wa maelezoa ya Dk. Shein idadi ya kesi za ujauzito wa wanafunzi zilizoripotiwa zimeongezeka kutoka 19 mwaka 2015 na kufikia 26 mwaka 2016 zikijumuisha wanafunzi kutoka darasa la 6 hadi kidato cha 4 pia, kesi za ndoa za wanafunzi nazo zimeongezeka kutoka 14 mwaka juzi hadi 25 mwaka jana. Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema kuwa kujengwa kwa skulin hiyo kutaondosha ufumbufu kwa wananfunzi waliokuwa wakifuata skuli mbali na sehemu wanazoishi. Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Khadija Bakari Juma akitoa maelezo juu ya skuli hiyo alisema kuwa mradi wa ujenzi wa skuli hiyo ya Sekondari ya Kwarara na Kiutuo cha Habari unatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wananchi na Watu wa Jamhuri ya Korea kupitia mashirika mbali mbali ya maendeleo. Alisema kuwa ujenzi huo ni wa majengo mawili moja ni kituo cha Habari za elimu na Skuli ya Sekondari ambayo ina madarasa 12 Ofisi ya Walimu, Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Maktaba, chumba cha Mkutano, chumba cha Kompyuta, chumba cha ushauri nasaha, voo, maabara na ina uwezo wa kuchukua wanafuzi 1080 kwa mikupuo miwili. Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa Kituo hicho cha Habari kitaandaa na kutoa vipindi mbali mbali vya elimu ambavyo vitawalenga walimu, wanafunzi na jamii wa skuli zote za Unguja na Pemba ambapo vipindi hivyo vinatarajiwa kurushwa kupitia SUZA TV na SUZA Radio ambayo ilizinduliwa hivi karibuni. Nao viongozi wa Mashirika hayo ya misaada kutoka Korea kwa nyakati tofauti walieleza azma yao ya kuenmdelea kutoa ushirikiano wake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu na sekta nyengine hapa nchini. Kabla ya hafla hiyo viongozi hao kutoka Korea walifanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar ambapo Dk. Shein alitumia fursa hiyo alitoa pongezi kwa Jamhuri ya Korea kupitia Mashirika yake kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi hizo za Mashirika hayo ya Korea katika kuunga mkono harakati za maendeleo hapa Zanzibar na kueleza kuwa mradi wa skuli ya Kwarara ni wa mwazo katika miradi ya elimu ambayo haijawahi kutokea. Dk. Shein alisema kuwa Tanzania na Jamhuri ya Korea zilianza mahusiano ya Kidiplomasia mnamo mwaka 1999 ambapo nchi hiyo imeweza kuisaidia Tanzania ikiwemo Zanzibar mambo mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu, kuimarisha kilimo cha mpunga, kilimo cha umwagiliaji maji na hivi karibuni mradi wa kufuga samaki nao unatarajiwa kuanza. Katika mradi huo mpya wa kufuga samaki Dk. Shein alisema kuwa umradi huo utazalisha vifaranga vya samaki na majongoo ya bahari utakaogharamiwa na KOICA. Shirika la SBS lilieleza kuwa mikakati yao ni kujenga skuli mia moja katika bara la Afrika na skuli hiyo ya Kwarara ni ya Miamoja kati ya 99 ambazo wamejenga katika nchi nyengine ila kwa upande wa skuli hiyo ni ya kipekee kutokana na kuwa na studio na mambo mengine ya habari, mradi ambao KOICA nao wamesaidia kwa asilimia 50. Sambamba na hayo, Shirika la KOICA linatarajia kutoa msaada wa dola za Kimarekani milioni 10 ambazo zitapitia kwa Shirika lisilo la Kiserikali la Korea kwa ajili ya kuimarisha elimu ya Sekondari kwa wanafunzi wa kike na Shirika la Good Neighbors Tanzania wamekubali kujenga skuli ya msingi huko Kwarara itakayokuwa na madarasa 24 ambapo tayari eneo la skuli hiyo limeshapatikana. Shirika la SBS TV limeadihi kuitangaza Zanzibar nchini mwao sambamba na kuutangaza utamaduni wa Zanzibar kutokana na vipindi maalum vya Televisheni watakavyovitengeneza ambapo pia uongozi huo ulimpongeza Dk. Shein kwa juhudi zake za kuchapa kazi .
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo