Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Waziri Mkuu Majaliwa afungua Saccos ya meli nne Zanzibar
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Meli nne saccos kuhakikisha wanakuwa wawazi na kutoa taarifa za hesabu za umoja huo kila wakati ili wanachama waweze kuwa na takwimu sahihi. Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizindua saccos hiyo yenye mtaji wa zaidi ya sh. bilioni moja kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinguzi Matukufu ya Zanzibar. Waziri Mkuu alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa wawazi kwa wanachama wenzao jambo ambalo litawajengea uaminifu hivyo kuwezesha umoja huo kudumu na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Alisema vyama vingi vya ushirika nchini vimekufa kutokana na viongozi wake kutokuwa waaminifu hivyo Serikali hatokubali kuona suala hilo linatokea katika umoja huo kwani litakwamisha maendeleo. Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha saccos hiyo kwani wameweza kutimiza ndoto ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ya kuondokana na umasikini, dhuluma na unyonge. Waziri Mkuu alisema saccos hiyo itawawezesha baadhi ya wanachama kuanzisha miradi ya ujasiriamali na wengine kuongeza mitaji hivyo kukuza biashara zao na kuondokana na umasikini. Awali, Waziri Mkuu alizindua ukumbi wa kisasa wa mikutano unaomilikiwa na saccos hiyo na kuwapongeza wananchi hao kwa kubuni miradi ya maendeleo itayowaongezea kipato na kuweza kujikwamua kiuchumi. Hata hivyo aliwataka wanachama hao kuendeleza mshikamano wao na kuendelea kushirikiana na Serikali ambayo imejipanga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo ya ujasiriamali hasa kwa walio katika vikundi vya uzalishaji. Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwashauri wanachama wa umoja huo kufikiria uwezekano wa kuanzisha viwanda ili kukuza mitaji yao. Pia vitawezesha umoja kuongeza za fursa za ajira nchini. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, ALHAMIS, JANUARI 12, 2017.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo