Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Azindua Jengo la Zimamoto Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitahadharisha kwamba uzembe wa aina yoyote unaoweza kufanywa na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi wakati inapotokea dharura kwa bahati mbaya unaweza kukimbiza huduma za ndege za Kimataifa zinazotumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Alisema umuhimu wa Kikosi hicho kuwepo katika maeneo ya Viwanja vya ndege hata Bandarini kwa ajili ya kutoa huduma za uokozi wa masuala ya dharura ni muhimi na mkubwa kwa Uchumi wa Taifa hili. Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964. Balozi Seif alisema Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada mbali mbali za kukiimarisha Kikosi hicho cha Zimamoto ili kiende sambamba na Teknalojia ya kisasa pamoja na kufikia kutoa huduma zenye viwango vya Kimataifa. Alisema Idara ya Zimamoto na uokozi ni nyenzo muhimu katika Taifa lolote Duniani, hivyo ni vyema kwa watendaji wa Taasisi hiyo wakaandaliwa utaratibu muwafaka wa kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ndani na nje ya nchi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa wito kwa watendaji wa Kikosi hicho kutoa mafunzo maalum kwa watendaji wa Serikali, Taasisi za Umma na hata zile binafsi katika kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea katika maeneo yao ya kazi. Aidha Balozi Seif aliuomba Uongozi wa Taasisi hiyo kushirikiana na Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar katika kutoa mafunzo maskulini juu ya suala zima la Zimamoto na Uokozi ili kutengeneza jamii yenye ufahamu na utayari katika kukabiliana na majanga wakati yanapotokezea. Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza Makamanda na wapiganaji wa vikosi vya ulin zi na usalama hapa Nchini kwa jitihada mbali mbali wanazochukuwa katika kukabiliana na maafa katika sehemu mbali mbali hapa Nchini. Alieleza kwamba Wananchi wengi hivi sasa wamejenga imani kubwa kwa Vikosi hicho, hivyo ni vyema wakaendelea kujiaminisha kwa Jamii iliyowazunguuka wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho, Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Kamishna Ali Abdulla Malimus alisema kituo cha Zimamoto na Uokozi kiliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amain Karume kimejengwa kwa kuzingatia vigezo vya Kimataifa kufuatia agizo la Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein. Kamishna Ali Abdulla alisema askari wa Kikosi hicho wameonyesha faraja yao kutokana na jitihada kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuimarisha miundombinu na Vifaa vya kisasa kwa kikosi chao vinavyolingana na uwezo wa huduma zinazohitajika kutolewa kwenye Viwanja vya ndege. Alieleza kwamba kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Aman Karume Zanzibar hivi sasa kimekuwa na harakati kubwa za kuhudumia ndege kubwa za Kimataifa kutoka Mataifa mbali mbali Duniani. Kamishna wa Zimamoto na Uokozi Zanzibar alisema Kikosi hicho tayari kimeshapokea magari makubwa ya Kisasa Mawili kati ya Manne yaliyonunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitia Mradi salama ambao kila gari Moja lina uwezo wa kutoa Lita 9,000 kwa dakika moja wakati wa kutoa huduma za dharura. Hata hivyo Kamishna huyo alieleza changamoto ya sasa inayokikabili Kikosi hicho kuwa ni uhaba wa watendaji wenye elimu na Taaluma Maalum inayoweza kukidhi mahitaji ya kupambana na Majanga makubwa kama ajali za Ndege kubwa zinazoruka na kutua. Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Bibi Radhia Rashid Haroub alisema ujenzi wa Kituo hicho cha Zimamoto na Uokozi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uliojumuisha Taasisi tofauti za Umma umeigharimu Serikali Kuu jumla ya Shilingi Milioni 234,000,000/-. Bibi Radhia alisema Kituo hicho kina sehemu maalum ya maegesho ya Magari ya Kikosi hicho, Ofisi ya Mkuu wa Kituo, Chumba cha Mawasiliano pamoja na Vyumba wa Askari wanawake na wanaume. Akimkaribisha Balozi Seif kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jengo la Kituo cha Zimamoto Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali ya Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Shamata Shaame Khamis alisema Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kimeongezewa nguvu ya utekelezaji wa majukumu yake iliyopangiwa kila siku. Mheshimiwa Shamata alisema nguvu hizo za miundombinu na vifaa ni miongoni mwa malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuzipatia uwezo Taasisi zake ikitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo