Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Kikao cha Kamati ya pamoja ya Serikali ya SMT na SMZ kuhusu masuala ya Muungano
Kikao cha kamati ya pamoja ya Viongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu masuala ya Muungano kimekutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. Wajumbe wa Kiko hicho ambao ni Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu , Watendaji na baadhi ya Wataalmu wa pande zote mbili za Tanzania walikutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi wa zamani uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar. Akiwasilisha Taarifa ya Maazimio ya Kikao cha Mawaziri wa SMT na SMZ Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira na Muungano Mh. Januari Makamba alisema kikao hicho kilijadili Agenda 10 na Mada Mbili. Mh. Makamba alisema moja ya miongoni mwa agenda Kuu za Vikao hivyo ni ile ya chimbuko la changamoto za Muungano ambazo baadhi zilizokuwa zikileta kero pande zote za Muungano tayari zimeshapata ufumbuzi na nyengine ziko katika mchakato wa kuzitanzua. Alisema ushiriki wa pamoja wa wataalamu na watendaji waandamizi wa pande mbili za Muungano katika vikao vya kujadili changamoto zinazolalamikiwa na sehemu zote husika kuanzia ngazi ya chini na kuwasilishwa kwa Makatibu Wakuu na hatimae Mawaziri wa pande hizo umesaidia kupunguza kero hizo. Waziri Januari Makamba alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto, Gharama za deni la Tanesco kwa Zeco, utumishi wa wafanyakazi wa Zanzibar kwa Taasisi za Muungano, uvuvi wa bahari kuu pamoja na Zanzibar kutofaidika na miradi iliyoanzishwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Alieleza kwamba yapo baadhi ya masuala kimsingi yanayohitaji utaratibu wa kubadilishwa kwa baadhi ya Sheria kwenye Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye yaridhiwe na Baraza la Wawakilishi akilitolea mfano lile la Uvuvi wa Bahari Kuu. Akichangia kwenye kikao hicho Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa kuandaa utaratubu mzuri wakati wa ujio wa Viongozi Wakuu wa Mataifa ya Nje wanaofanya ziara Nchini Tanzania na hatimae pia kufika Zanzibar. Mh. Majaliwa alisema utaratibu huo ambao ulikuwa ukitumika siku za nyuma ni vyema ukawasilishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili ipate fursa ya kujipanga mapema jinsi inavyoweza kufaidika na ujio wa Viongozi hao wa Kimataifa. Waziri Mkuu Majaliwa aliwaeleza wajumbe wa Kikao hicho kwamba katika azma ya kuhakikisha Muungano wa Tanzania unaimarika kwa pande zote mbili utaratibu wa Viongozi Wakuu wa Upande wa Tanzania Bara umeshaandaliwa wa kufanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo kwa upande wa Zanzibar. Alisema wapo baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tayari wameshafanya ziara kama hizo hasa wale wanaohusika na Wizara za Muungano zenye Taasisi zake upande wa Zanzibar, akamtolea Mfano Waziri wa Mambo ya Ndani. Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitahadharisha kwamba wapo baadhi ya watu wasioutakia mema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao tayari umeshatimiza miaka 53 sasa. Balozi Seif alisema watu hao hutumia mapungufu na changamoto zilizopo katika baadhi ya kero za Muungano kwa kupotosha Wananchi kwa makusudi dhamira halisi na malengo la Muungano ambayo ni Umoja na Mshikamano wa Wananchi wa pande zote mbili. Akikiahirisha Kikao hicho Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan alisema kitendo cha Serikali zote mbili kuwatumia Wataalamu wao katika ngazi ya msingi kwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto za Muungano kimesaidia kuleta suluhu na ufumbuzi wa mambo mengi. Hata hivyo Mh. Samia alisema kutokana na mabadiliko ya dunia yanayokwenda kwa kasi katika harakati za Kimaisha katika mfumo wa teknologia ya Kisasa ya Habari na Mawasiliano changamoto za Muungano bado zitaendelea kuibuka nyengine. Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyofikia ya kupitisha sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar baada ya Bunge la Muungano kupitisha sheria ya kuiwezesha Zanzibar ijitegemee yenyewe katika masuala hayo. Mh. Samia alieleza kwamba Wananchi wasingependa kuona suala la mafuta na Gesi asilia linarejea tena kwenye masulala yanayoleta kero ndani ya Muungano wa Tanzania.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo