Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wafanyakazi wa Serikali kulipwa kima cha chini TZS 300,000 kuanzia mwezi April mwaka huu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa mipango yote imekamilika ya kuwalipa wafanyakazi wa Serikali kima cha chini cha mshahara kwa asilimia mia moja kutoka TZS 150,000 hadi TZS 300,000 kuanzia mwezi April mwaka huu. Hatua hiyo ni kuyaenzi na kuyatunza Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 ambapo Dk. Shein alisema hayo leo huko katika uwanja wa Amaan mjini Unguja wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofika katika maadhmishi ya kilele cha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Dk. Shein alisema kuwa Serikali, katika mwaka 2016, imeshughulikia nidhamu za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria Nam. 2 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2011 na Kanuni za Kazi. Alisema kuwa wapo watumishi walioondoshwa kwenye dhamana za uteuzi kwa kukiuka maadili ya kazi, vile vile, wapo waliosimamishwa kazi kutokana na ubadhirifu wa mali za umma na wanaendelea kuchunguzwa na kushughulikia na taasisi zinazohusika. Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kuwa katika kipindi hiki, Serrikali imesimamia udhibiti wa matumizi ya fedha za umma kwa kupunguza safari za nchi za nje na za ndani ya nchi kwa watumishi wa umma, mikutano, semina na makongamano yamefanyika bila ya wahusika kulipwa posho katika wakati wa kazi. Alieleza kufarajika kwake kuona wananchi wa Zanzibar wameungana na Serikali yao katika kipindi cha miaka 53 kwa kuyatekeleza malengo ya Mapinduzi na kupatikana mafanikio makubwa ya maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Dk. Shein alisema kuwa mafanikio yanayoonekana ya kuimarika kwa huduma mbali mbali yametokana na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka 2016. Sambamba na hayo, Dk. Shein alisema kuwa sekta ya biashara imeimarika pamoja na kusimamia biashara ya karafuu kupitia Shirika la ZSTC huku akieleza malengo ya serikali katika kipindi hiki cha pili cha awamu ya Saba kuwa ni kuimarisha viwanda. Kwa kushirikiana na wawekezaji na wafanyabiashara, Serikali imeanza kuchukua hatua ya ujenzi wa Ukanda wa Darajani na Michenzani, ‘Mapinduzi Square’ ambapo yatajengwa maduka ya biashara, maeneo ya kuegesha gari, kumbi za mikutano, ofisi na mambo mengineyo. Alieleza mafanikio katika sekta ya utalii, elimu, kilimo, ufugaji huku akieleza Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuendeleza sekta ya uvuvi ambapo maandalizi ya kuanzisha mradi wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya samaki huko Beit el Ras, yamefanikiwa. Alisema kuwa kudumisha kwa Mapinduzi ya Zanzibar ambayo leo yametimiza mika 53, lazima hatua hiyo iende sambamba na kudumishwa na kuendelezwa kwa Muungano wa Tanzania ambao ifikapo tarehe 26 April mwaka huu utatimiza mika 53 tokea kuasisiwa kwake. Alisema kuwa Siri kubwa ya mafanikio yanayoendelea kupatikana hapa nchini ni kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu na kuwataka wananchi wasichoke kuhimizana juu ya umuhimu wa amani, ili nchi iweze kupiga hatua zaidi katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi. Nae Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, alitoa pongezi kwa wananchi wa Zanzibar kwa kuazimisha miaka 53 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na kueleza azma ya Mapinduzi. Mapema Dk. Shein alipokea salamu za Rais na Mizinga 21 kupigwa ambapo Kamanda wa Gwaride alimkaribisha Rais Dk. Shein kukagua gwaride na baadae alipokea maandamano ya wananchi kutoka Wilaya za Unguja Pemba, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na wanafunzi wa Vyuo. Gwaride lilipita mwendo wa pole na wa haraka haraka na kutoa heshima huku maonesho maalum ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Polisi huku Makomandoo wakionesha ustadi wao sambamba na hali ya ulinzi kwa kutumia mbwa na farasi.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo