Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Serikali ya Zanzibar Inakusudia Kuimarisha Sekta ya Uvuvi Katika Azma ya Kujenga Uchumi Imara.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuimarisha Sekta ya Uvuvi katika azma yake ya kujenga uchumi imara unaojitegemea utakaostawisha maisha ya Wananchi wake. Alisema uimarishaji huo utaelekezwa zaidi katika ujenzi wa Viwanda Vidogo vidogovya usindikaji wa mazao ya Baharini utakaotoa fursa ya kukaribisha Makampuni na Taasisi za Kimataifa kuwekeza miradi yao Visiwani Zanzibar. Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong kutoka Nchini China ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Bwana Lan Ping Yong hapo Ofisini kwake Majengo ya Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Alisema Sekta ya Uvuvi bado ina rasilmali ya kutosha inayoweza kusaidia uchumi wa Taifa unaokwenda sambamba na fursa za upatikanaji wa ajira zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya Wananchi walio wengi Nchini. “ Hii ni njia bora na mwafaka ya upatikanaji wa ajira hasa kwa Vijana ”. Alisema Balozi Seif Ali Iddi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza ujumbe wa Viongozi wa Kampuni hiyo ya Hong Dong ambao amewahi kukutana nao wakati wa ziara yake ya Kiserikali ya hivi karibuni Nchini China kwamba juhudi zitafanywa na Serikali katika kuona azma ya Kampuni hiyo ya kutaka kuwekeza Zanzibar inafanikiwa. Balozi Seif alimuahidi Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Hong Dong na Ujumbe wake kuwa pande zinazohusika nchini zitakutana na kuangalia wazo la Kampuni hiyo la uwekezaji kwa lengo la kuchukuliwa hatua za muelekeo wa uanzishwaji wa uwekezaji huo. Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong ya Nchini China Bwana Lan Ping Yong alisema mradi wa Uvuvi unaotaka kuwekezwa Visiwani Zanzibar utakuwa na uwezo wa kutoa fursa za ajira zisizopungua elfu 1,700. Bwana Ping alisema licha ya nafasi za ajira zikilengwa kwa Wazalendo lakini pia utaambatana na wataalamu wa Kampuni ya Hong Dong kutoa mafunzo ya Uvuvi kwa Wavuvi wa Kienyeji ili waendeshe miradi yao katika Mfumo wa Kisasa unaokubalika Kimataifa. Bwana Ping alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyokwisha patikana katika Nchi ya Mauritania iliyoko Magharibi ya Bara la Afrika baada ya Kampuni hiyo kuwekeza Mradi wa Uvuvi Nchini humo. Alisema mapato ya Wavuvi wadogo wadogo wa Nchi hiyo waliobahatika kuwemo kwenye mradi huo kwa sasa yameongezeka na kuleta ustawi wa familia zao na Taifa lao kwa ujumla. Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Hong Dong alisema Taasisi hiyo imetenga nafasi Tatu kwa ajili ya Watendaji wa Sekta ya Uvuvi Zanzibar kwenda Nchini Mauritania kujifunza hatua iliyofikia ya Uwekezaji wa Kampuni hiyo katika Nyanja ya Uvuvi. Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana J. C. Barupal Ofisini kwake katika Majengo ya Baraza la Wawakilishi Mbweni Wilaya ya Magharibi “B”. Katika mazungumzo yao Balozi Seif alisema Nchi ya India iliyopo Bara ya Asia imeshapiga hatua kubwa katika masuala ya Teknolojia ya kisasa ambayo Zanzibar kama Nchi inayoendelea inaweza kujifunza kwa kina Taaluma hiyo kutoka kwa Walaalamu wa India. Balozi Seif alimueleza Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar kwamba Makampuni ya India yana uwezo wa kuanzisha miradi yao katika sekta za Kilimo, Biashara na Viwanda Visiwani Zanzibar ili kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukaribisha Vitega uchumi vya miradi tofauti Nchini. Naye kwa upande wake Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana J.C. Barupal alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba India itaendelea kuunga mkono harakati za maendeleo ya Zanzibar. Bwana Barupal alisema uungaji mkono huo umekuja kufuatia mafungamano ya muda mrefu yaliyopo ya Ushirikiano wa Kihistoaria kati ya pande hizo mbili hasa katika masuala ya Kibiashara yaliyotoa fursa kwa wafanyabaishara wa India kuingiza bidhaa zao Visiwani Zanzibar karne nyingi zilizopita nyuma.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo