Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Rais wa Zanzibar Dk Shein Awataka Wananchi Kupuuza Uvumi Unaoenezwa. Katika Mitandao ya Kijamii. Hakuna Baraza la Wawakilishi Linalovunjwa Katika Mwaka Mmoja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa yeye ndio Rais wa Zanzibar na kueleza kuwa hakuna Baraza la Wawakilishi linalovunjwa ndani ya mwaka mmoja na kiutaratibu Baraza hilo huvunjwa baada ya miaka mitano kwa sheria, taratibu na kanuni zake. Hivyo Dk. Shein aliwataka wananchi na wanaCCM kuepuka kauli za upotoshwaji zinazosambazwa mitandaoni. Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika ukumbi wa CCM, Mkoa wa Mjini iliopo Amani mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mpira wa Miguu kwa Timu 18 za Unguja. Katika maelezo hayo Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayoiongoza yeye itaendelea kuwa madarakani na kueleza kuwa mazungumzo aliyoyafanya leo kati yake na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni mazungumzo ya kawaida baada ya kumwita kwa lengo la kubadilishana mawazo na kueleza changamoto zilizpo katika Majimbo yao. Dk. Shein alisema kuwa yeye akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi pia, ni sehemu ya Baraza hilo na kwenda kuzungumza na Wajumbe wa Baraza hilo sio jambo jipya kwani ameshawahi kufanya hivyo kutokana na taratibu na kanuni zilizopo. Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwasisitiza wanaCCM na wananchi kuwa hakuna Baraza linalovunjwa asubuhi hivyo kauli hizo zinazozungumzwa na zinazosambaa ni za upotoshaji na zisizo na ukweli. Aidha, Dk. Shein aliwaeleza wanaCCM wakiwemo vijana waliohudhuria katika hafla hiyo kuwa Mihimili mitatu iliyopo ikiwemo Mahakama, Serikali na Baraza la Wawakilishi hakuna muhimili hata mmoja unaomshurutisha mwenziwe bali hufanya kazi kwa mashirikiano ya pamoja ili kufikia malengo yaliokusudiwa katika nchi. Nae Balozi Seif Ali Idd Makamo wa Pili wa Rais alieleza kuwa uzushi unaosambazwa katika mitandao hauna maana na kueleza kuwa amepokea simu nyingi kutoka kwa wananchi kutokana na kauli hizo za mitandaoni ambazo si za msingi kuwa Dk. Shein leo anakabidhi nchi kwani maneno hayo hayakuanza leo bali ni kawaida kwa wapinzani. Hivyo aliwataka wanaCCM na wananchi kupuuza kauli hizo. Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo