Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Hospitali ya Kivunge na Makunduchi kupandishwa hadhi kuwa za Mkoa katika kipindi kifupi kijacho.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuzipandisha hadhi Hospitali ya Kivunge na Makunduchi kuwa za Mkoa katika kipindi kifupi kijacho. Dk. Shein aliyasema hayo katika chakula cha usiku kilichoandaliwa na Wizara ya Afya kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Hospitali ya Kivunge ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za afya Zanzibar (HIPZ), huko katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatt mjini Zanzibar. Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa juhudi za Mradi wa kuendeleza huduma za afya Zanzibar (HIPZ), sio tu umeweza kusaidia kuziweka hospitali za Makunduchi na Kivunge katika hali nzuri na bora katika utoaji wa huduma lakini amesema mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa uongozi wa Mradi huo wa HIPZ kwa kuweza kuimarisha huduma za afya, miundombinu, usimamizi na uwajibikaji katika Hospitali hizo. Aliongeza kuwa Mradi wa HIPZ umesaidia sana kutekeleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuzifanya Hospitali hizo kuwa na hadhi ya Hospitali ya Wilaya hali ambayo imeonesha njia ya kutekeleza lengo la kuzifanya Hospitali hizo kuwa za Mkoa. Aidha, Dk. Shein alitoa wito kwa Wizara ya Afya kuimarisha utoaji mafunzo kupitia Maradi huo kwa madaktari wazalendo kupitia madaktari wageni wanaokuja kufanya kazi Zanzibar kupitia katika Mradi huo wa HIPZ. Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuzitumia huduma zinazotolewa na wataalamu wa HIPZ kupitia Hospitali ya Kivunge na Makunduchi badala ya kukimbilia Hospitali Kuu ya MnaziMmoja. Dk. Shein katika alieleza juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya, ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee, Hospitali ya Mnazi Mmoja, kuimarisha miundombinu ya hospitali, vifaa na mafunzo huku akieleza kuwa Serikali imeongeza Bajeti ya Wizara ya Afya kutoka Tsh. Bilioni 4.3 mwaka 2015/2016 hadi kufikia Bilioni 4.9 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017. Katika maelezo yake kwenye hotuba hiyo Dk. Shein alisema kuwa Mradi huo wa HIPZ umeimarishwa kwa mashirikiana kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzbar pamoja na madaktari kutoka nchini Uingereza, Canada na sehemu nyengine duniani. Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwaahidi viongozi wa Mradi huo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Znzibar itaendea kuwaunga mkono ili Mradi huo uwe endelevu na uweze kufanya kazi vizuri. Alitumia fursa hiyo pia, kuwashukuru Washirika wa maendeleo kwa kuendeleza aushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za afya. Katika hafla hiyo jumla ya Tsh. Milioni 67 zilichangwa katika harambee ilioendeshwa ukumbini hapo ambapo Dk. Shein alichangia milioni kumi pamoja na Mama Mwanamwema Shein nae alichangia milioni tano. Nae Waziri wa Afya, Mahamoud Thabit Kombo kwa upande wake alieleza mashirikiano mazuri yaliopo kati ya HIPZ na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Afya na kumpongeza Rais Dk. Shein kwa kuwa kiungo kati Wizara hiyo na Mradi huo wa HIPZ. Nao viongozi wa HIPZ kwa nyakati tofauti walieleza mafanikio na changamoto walizokabiliana nazo ndani ya miaka kumi ya Mradi huo na kuahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kuimaruisha sekta ya afya hapa nchini. Sambamba na hayo walieleza mashirikiano mazuri waliyoyapata kutoka Serikalini pamoja na kutoka kwa washirika mbali mbali wa maendeleo. Mradi wa HIPZ ulianzishwa mwaka 2006 ambao unafanyakazi chini ya Wizara ya Afya ili kuimarisha huduma zote za afya za Hospitali ya Makunduchi na Kivunge. Viongozi mbali mbali walihudhuria katika hafla hiyo akiwemo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd, Mama Asha Balozi, Mawaziri, viongozi Serikali na viongozi wa HIPZ wakiongozwa na Dk. Ruaraidh Mac Donagh pamoja na wageni wengine.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo