Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Hakuna mtu anaeweza kumg’oa Dk.Shein katika nafasi yake ya Urais wa Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa yeye ndie Rais halali wa Zanzibar aliyechaguliwa kwa kishindo na wananchi wa Zanzibar na kuapishwa kisheria hivyo hakuna mtu anaeweza kumg’oa katika nafasi yake hiyo. Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali ya ndani na nje ya Zanzibar, Ikulu mjini Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja wa kipindi cha pili cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba, chini ya uongozi wake. Katika maelezo yake Dk. Shein alieleza kuwa nafasi ya urais hupatikana kwa kufanyika kwa uchaguzi na chama chake kimeingia kwenye uchaguzi na wananchi walio wengi wamemchagua na kupata ushindi wa kishindo na kuweza kuendelea katika nafasi yake hiyo na baada ya ushindi wake hatua zote za kisheria zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuapishwa kuwa Rais na Jaji Mkuu wa Zanzibar. Hivyo, alishangazwa na kauli zinazoenezwa kuwa nafasi yake hiyo kuna kiongozi anapita akiwaeleza wananchi kuwa itachukuliwa na kiongozi huyo ambapo alihoji kuwa amechaguliwa na nani na vile vile ataapishwa na nani na kwa utaratibu na sheria zipi na za wapi. Alieleza kuwa yeye ameshinda kihalali uchaguzi na pia ndio kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivyo yoyote mwenye ubavu zaidi ya Katiba na Sheria zilizopo nchini basi akamuondoshe katika nafasi yake hiyo. Mapema Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio yaliopatikana ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake na kusisitiza kuwa hali ya amani na utulivu imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha kwa uchumi. Alisema kuwa ukusanyaji wa mapato Serikali imekusanya jumla ya TZS milioni 504,709 kwa kipindi cha Machi, 2016 hadi Februari 2017 kati ya hizo TZS milioni 249,279 zilikusanywa na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Na (TRA) ilikusanya TZS milioni 200,840. Kwa upande wa sekta ya elimu alisema kuwa elimu ya juu imeimarishwa, wanafunzi wa vyuo vikuu wameongezeka kutoka 6370 katika mwaka 2015 hadi kufikia 7,303 katika mwisho mwa mwaka 2016 ambapo mikopo ya elimu ya juu imetolewa kwa wanafunzi 2655 kwa jumla ya TZS bilioni 3.7. Pia, Dk. Shein alieleza kuimarika kwa sekta ya afya, miundombinu ikiwemo barabara, pamoja na juhudi zinazochukuliwa na Serikali anayoiongoza katika kuimarisha sekta ya maji safi na salama. Dk. Shein alieleza azma ya MV Mapinduzi II kufanya safari zake Comoro, Mombasa, Mtwara na Msumbiji ambapo hivi karibuni itaanza safari zake huko Comoro. Pia, kwa upande wa sekta ya kilimo alieleza mafanikio na mikakati iliyowekwa katika kuimarisha sekta hiyo. Kuhusiana na ujenzi wa bandari mpya ya Mpiga duri Dk./ Shein alisema akuwa Serikali ipo hatua za mwisho za matayarisho ya kuanza kwa ujenzi huo ambapo hatua za uchunguzi wa udongo imekamilika na kinachosubiriwa ni idhini ya matumizi ya fedha kutoka BENKI YA exim YA China ili kazi hiyo ianze chuni ya usimamizi wa Kampuni ya Ujenzi ya China Harbor Engineering Company, CHEC. Akueleza kuhusu sekta ya mafuta na gesi Dk. Shein alisema kuwa Serikali itafaidika kwa kiasi kikubwa na hatua hiyo ambayo kwa hivi sasa shughuli ya utafutaji unafanywa na kampuni ya Bell Geospace Enterprises Limited ya Uingereza kwa niaba ya Kampuni ya Rak Gas ya Ras Al Khaimah. Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza hatua za uimarishaji wa sekta ya habari na kueleza azma ya kuvifanya vyombo vya habari vya SMZ kuwa na hadhi ya vyombo vya Serikali. Kwa upande wa sekta ya michezo alieleza azma ya Serikali kujenga viwanja vya michezo kwa kila wilaya ambapo tayari kwa Wilaya ya Kusini kiwanja cha Kitogani kimeanza kujengwa. Ambapo pia, Dk. Shein aliendelea kusisitiza kuwa ZFA juhudi zake ielekeze katika kusiamamia mpira wa miguu na kuepuka masuala ya mpira kwenda mahakamani na badala yake yatatuliwe kwenye chombo cha mpira kwani CAF haiutambui utaratibu huo.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo