Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Balozi Seif Awaasa Wafanyakazi Wanapaswa Kujituma Katika Majukumu Yao ya Kazi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wafanyakazi wanapaswa kujitahidi kutekeleza majukumu yao ya Utumishi wa Umma kwa kufanya kazi kizalendo na ushirikiano uliotukuka ili kujijengea mazingira bora ya hatma yao ya baadae. Alisema tabia hiyo njema itawapa heshima kubwa katika Jamii kiasi wamba wamalizapo muda wao wa Utumishi watajikuta wakiacha athari inayoendelea kukumbukwa kwa wema na watumishi wenzao waliowaacha. Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuwapongeza na kuwaaga Wafanyakazi 13 waliostaafu kati ya Mwaka 2015/2016 na 2016/2017 wa Idara tofauti zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar. Alisema haipendezi na ni hulka mbaya inayowakumba baadhi ya Watumishi wa Umma hawa wale wenye mardaraka pale wanapofikia muda wao wa kustaafu na walio nyuma yao wakasherehekea kwa Pilau kutokana na vitendo vyao vilivyokosa imani kwa kutowatendea haki. Balozi Seif aliwapongeza Wafanyakazi wote waliostafu kwa kumaliza Utumishi wao katika njia ya salama na afya njema iliyopatikana kwa wao kuzingatia na kufuata mashauri ya Kitaalamu ya Afya katika mfumo wa kufanya mazoezi baada ya muda wa kazi. Aliwataka wafanyakazi wanaofikia umri wa kustaafu kuachana na tabia ya kujenga hofu kipindi wanachokaribia kumaliza muda wao wa Utumishi kwani kinaweza kuwasababishia msongo wa mawazo yanayoishia kupata maradhi. Balozi Seif alitanabahisha wazi kwamba kustaafu sio mwisho wa maisha lakini kinachotakiwa kwa wastaafu hao ni kujipanga vyema ili kukabiliana na mabadiliko ya maisha mapywa wanayoyaingia. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wafanyakazi wapya na wale wanaoendelea na utumishi wao kutumia maarifa, uzoefu, ujuzi na hata mbinu zilizokuwa zikitumiwa na watangulizi wao waliostaafu ili kupata ufanisi mzuri kwa Wizara na Taifa kwa ujumla. Mapema akitoa Taarifa fupi ya wafanyakazi hao wastaafu, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bibi Halima Ramadhan Toufiq alisema Utumishi wa Wafanyakazi hao wastaafu katika Taasisi za Umma umesaidia kizazi kipya katika kuendeleza gurudumu waliloliacha. Bibi Halima alisema licha ya wastaafu hao kuwa na uwezo kamili wa kuwajibika zaidi lakini Kifungu cha 68 {1} cha Utumishi wa Umma kimeweka bayana kuhusu kumaliza kwa Mkataba wa ajira. Mkurugenzi huyo wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wastaafu hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wapya ili kuwapa maarifa yatakayowasaidia kumudu vyema kutekeleza kazi zao. Bibi Halima aliwataja Wafanyakazi hao 13 wastaafu kuwa ni pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Waziri Kiongozi na Ndugu Abdulla Ali Abdulla Kitole aliyekuwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Wengine aliowataja ni Nd. Khatib Said Khatib aliyekuwa Mkurugenzi Uratibu, Bibi Shinuna Idara ya Faradha, Nd. Makame Mussa, Nd. Hassan Mohamed Hassan , Nd. Tajo Hussein Mawele, Bibi Amina Hussein Haji, Maabad Mlekwa Maabad, Siende Khatib Khamis, Mafunda Khamis Hamad, Kiboga Suleiman na Aziza Khalef Mohamed. Wastaafu hao pamoja na mambo mengine walikabidhiwa vyetu maalum, zawadi mbali mbali kulingana na kada zao pamoja na fedha taslim kama ni ukumbusho kwao kutokana na utumishi wao mzuri uliotukuka. Akitoa shukrani kwa niaba ya Wastaafu wenzake 13 Mstaafu nambari moja katika kundi hilo Mama Asha Suleiman Iddi alikiasa Kikazi kipya kinachoingia katika ajira mpya iwe ya Umma na hata ya Sekta binafsi kuacha tamaa ya kutaka kujilimbikizia mali na utajiri ndani ya kipindi kifupi cha ajira zao. Mama Asha alisema kitendo hicho ambacho hushabikiwa na baadhi ya watu mitaani kwa kuonekana mjanja na mwenye maarifa mbali ya kuhatarisha ajira zao laikini pia kinakwenda kinyume na kanuni, maadili na heshima ya Kazi. Akizungumzia suala na viinua mgongo vya watumishi wastaafu Mama Asha aliziomba Taasisi zinazosimamia masuala hayo kufanya juhudi za ziada katika kuona haki za wastaafu hao zinapatikana kwa wakati muwafaka bila ya kuleta kughdha yoyote. Alisema zipo dalili zinazoonyesha kuwatia hofu baadhi ya watumishi wastaafu kutokana na kucheleweshewa masurufu yao ambayo tayari wameshalenga kuwaendelesha katika muda wao wa kumalizia maisha.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo