Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Mbunge wa Jimbo la Kiwengwa Akipiga Akabidhi Vyerehani Kwa Wanafunzi Wa Kituo cha Ushoni Kinduni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema njia pekee ya kukubalika kwa vyuo vinavyoanzishwa Nchini ni umahiri wa ufundishaji unaotokana na Walimu wenye ujuzi na sifa za kufundisha zitakazowashawishi watu kujiunga ili kupata maarifa ya kina. Alisema umahiri huo utaimarika vizuri zaidi iwapo Uongozi wa Taasisi husika utaamua Chuo chao kukisajili kwenye Mamlaka husika kutegemea fani ya usomeshaji jambo ambalo litakifanya Chuo kilichoanzishwa kutoa vyeti bora vitakavyokubalika katika soko la ajira. Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika hafla aliyowakilishwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziri Pembe Juma wakati akikizindua Rasmi Kituo cha Jamii Kinduni { Kinduni Community Center – KCC } kilichoanzishwa na Askari Wastaafu wa Wilaya ya Kaskazini “B” kililenga kutoa mafunzo ya ushoni, Komyuta, ufugaji, kilimo pamoja na Ulinzi. Alisema vyuo vingi vya miradi ya kujitegemea katika kazi za amali huanzishwa kwa makeke lakini baada ya muda mfupi husambaratika kutokana na ubadhirifu wa mali pamoja na udhaifu wa Uongozi unaowekwa mambo yanayowapa wakati mgumu Walimu kuendelea kufundisha kwa utulivu. Alitoa wito kwa Uongozi na Wanachama wa Kituo cha Jamii Kindi kutafuta watu wenye Taaluma ya kutosha kukiongoza Kituo hicho ili kuwa mfano bora wa vituo vya ujasiri amali vitakavyokuwa imara hapa nchini. Akiwapongeza Wanachama wa Kituo cha Jamii Kinduni kwa uamuzi wao wa kujenga jengo kwa nguvu zao ili kufanya shughuli zao za Maendeleo zitakazowasaidia kuimarisha harakazi zao za kimaisha katika kipindi hichi cha Kustaafu. Alisema uamuzi wao huo unaunga mkono sera ya Serikali inayowataka Wananchi kuunda vikundi vya kujiendeleza kimaisha badala ya kusubiri ajira Serikalini ambazo kwa sasa zina upungufu mkubwa sana. Alieleza kwamba wapo wastaafu wengi ambao hutaka kurudi tena Serikalini kuajiriwa upya lakini Wastaafu hao tayari wameshaona mitaani yapo mambo mengi ya kufanya yanayochangia kupunguza ukali wa Maisha katika wakati wa kustaafu. “ Kwangu mimi nyinyi ni chuo cha wastaafu wengine Nchini. Mmeweka mfano wa kuigwa na sisi tulioko Serikalini tutahakikisha ndoto yenu hii ya kujitegemea inakamilika na inazaa matunda mliyoyategemea ”. Alisema Balozi Seif. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru askari wote wastaafu Nchini kwa kulitumikia Taifa katika ngazi ya Ulinzi hadi kufikia kipindi chao cha kustaafu. Balozi Seif alisema mchango wa askari Wastaafu kwa Taifa hili hautosahauliwa daima kwa kipindi chote tokea Uhuru na Ukombozi ambapo Nchi imeendelea kuwa salama na wao ndio wachangiaji wakubwa wa kulifikisha hapa lilipo Taifa. Alisema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Majeshi yake imejijengea sifa kubwa Duniani kutokana na askari wake kuonyeha ukomavu katika ulinzi wa Kimataifa kwenye Mataifa mbali mbali Duniani. Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Viongozi wa Serikali na Kisiasa wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na Nje ya Mkoa huo kuendelea kuusaidia Umoja huo wa Askari Wastaafu ili uweze kufikia malengo uliojipangia wa Maendeleo. Akisoma Risala Mkurugenzi wa Umoja wa Wastaafu wa Wailaya ya Kaskazini “B” Ndugu Shabaan Mohamed Iddi alisema Umoja wao umepata mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake Mwaka 1992 kwa kubuni mipango mbali mbali ya miradi ya Maendeleo. Nd.Shabaan alisema hatua hiyo imekuja kufuatia dhamira yao ya kuunga Mkono kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuanzisha Vikundi vya Ujasiri Amali vinavyosaidia kuibua nafasi za ajira hasa kwa Vijana ili kuabiliana na ukali wa Maisha. Mkurugenzi huyo wa Umoja wa Askari Wastaafu wa Wilaya ya Kaskazini “B” alisema licha ya mafanikio hayo zipo changamoto zinazokwaza maendeleo ya haraka ya Umoja huo akizitaja baadhi kuwa ni pamoja na upungufu wa Vyarahani kwa darasa la Ushoni, ukosefu wa sanamni ndani ya Jengo lao jipya wanaloendelea nalo pamoja na huduma za Umeme. Nd. Shabaan aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Taasisi zake za Benki ya Watu wa Zanzibar {PBZ} na Wizara inayosimamia masuala ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuwapatia Mikopo itakayowawezesh kuendesha Miradi yao waliojipangia kwa ufanisi mkubwa zaidi. Akimkaribisha Mgeni rasmi kuzindua Kituo cha Jamii Kinduni iliyokwenda sambamba na Uzinduzi wa Jengo lao jipya Mwenyekiti wa Askari Wastaafu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Omar Bakar Yussuf amewashukuru Viongozi na Washirika wa Maendeleo walioamua kusaidia Umoja huo. Nd. Omar Bakari alisema misaada ya Viongozi na washirika hao imewawezesha Askari hao pamoja na Wanafunzi wao wa madarasa ya Ushoni, Kilimo, Kompyuta na Ulinzi kuendesha shughuli zao kwa ufanisi mzuri. Katika hafla hiyo Mh. Riziri Pembe Juma kwa Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikabidhi Vyarahani Vitano kwa Uongozi wa Askari hao Wastaafu wa Wilaya ya Kaskazini “B” kwa ajili ya Darasa la Ushoni la Kituo cha Jamii vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kiwengwa Mheshimiwa Khamis Mtumwa Ali.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo