Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Balozi Seif Azungumza na Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar. Alipofika Kujitambulisha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla lazima iendelee kubakia salama muda wote ili kuwapa fursa Wananchi, Wageni wanaoingia Nchini pamoja na Raia wake wafanye mambo yao ya kawaida bila ya bughdha yoyote. Balozi Seif alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Kamanda Mpya wa Brigedia Nyuki Zanzibar Brigedia General Fadhil Nondo aliyefika Ofisini kwake kujitambulisha Rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} hivi karibuni. Brigedia General Fadhil Nondo alikuwa akikaimu nafasi hiyo tokea Mwezi Januari Mwaka huu wa 2017 baada ya aliyekuwa akishikilia wadhifa huo Brigedia General Cyrill Ivor Mhaiki kufariki Dunia Mapema mwaka huu. Balozi Seif alisema Zanzibar inapaswa kuwa katika ulinzi wa uhakika muda wote kulingana na mazingira yake yaliyozunguukwa na Bahari ambayo wakati kwengine hutoa nafasi kwa wahalifu kufanya vitendo vinavyosababisha hofu na shaka kwa Wananchi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Brigedia Kamanda huyo wa Nyuki kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wake itakuwa tayari wakati wote kumpa ushirikiano wa karibu zaidi ili kuhakikisha anatekeleza vyema dhamana aliyokabidhiwa na Taifa. Hata hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake Balozi Seif alimshauri Brigedia General Fadhil Nondo kushirikiana na Makamanda na walinzi wa Vikosi vyengine vilivyopo Zanzibar ili kazi yao ya ulinzi iende vyema bila ya kukaribisha vikwazo, mikwaruzo au migongano yoyote ile isiyokuwa na faida. Balozi Seif alimtakia kheir na mafanikio katika uwajibikaji wake huo Mpya Kiongozi huyo Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} kwa upande wa Visiwa vya Zanzibar. Mapema Brigedia General Fadhil Nondo alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba atakuwa tayari kupokea maagizo yoyote atakayopewa kuyatekeleza katika nafasi yake hiyo mpya ya Uongozi. Kamanda Nondo alisema kwa mujibu wa Mfumo na Taratibu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania nafasi yake ya kazi inawajibika kutekelezwa kwa kupokea maagizo na ushauri kutoka kwa Viongozi wa Juu wa eneo analofanyia Kazi. Brigedia General Fadhil Nondo kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mafunzo na Operesheni wa Brigedia Nyuki pamoja na Mkuu wa Kambi la JWTZ iliyopo Bavuai Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo