Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Jeshi la Polisi Tanzania limepongezwa kwa kuendelea kusimamia vyema amani na utulivu hapa Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amelipongeza Jeshi la Polisi Tanzania, kwa kuendelea kusimamia vyema amani na utulivu hapa Zanzibar. Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Tanzania (IGP) Simon Nyakoro Sirro, aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwa Rais. Dk. Shein katika maelezo yake alimueleza IGP Sirro kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likifanya kazi kubwa katika kuhakikisha amani na utulivu inaimarishwa na wananchi wanajishughulisha na shughuli zao za kijamii wakiwa salama. Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa Jeshi la Polisi hapa Zanzibar limekuwa likitekeleza vyema kazi zake na kutoa mashirikiano mazuri kwa wananchi na kusisitiza kuwa ipo haja ya kuongeza ari hiyo ili liweze kuitumikia vyema jamii. Aidha, Dk. Shein alieleza imani yake na matumaini makubwa kwa uongozi wa IGP Sirro na kumuahidi kuwa ataendelea kutoa ushirikiano wake pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili Jeshi hilo lizidi kupata maendeleo sambamba na kusimamia vyema amani na utulivu hapa nchini. “Nataka nikuhakikishie kuwa Mimi na Rais Dk.John Pombe Magufuli tuna imani na matumaini makubwa na uongozi wako hasa tukitambua ari yako ya utendaji wa kazi, hivyo tunaimani kuwa Jeshi la Polisi litazidi kuimarika na mimi nakuahidi nitaendelea kukupa mashirikiano yote”,alisema Dk.Shein. Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza haja ya kuwepo mashirikiano ya kutosha kwa askari wa barabarani pamoja na taasisi husika inayotoa leseni za udereva wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali zisizo za lazima ambazo zimekuwa zikitokezea mara kwa mara. Dk. Shein alimueleza Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi kuwa kumekuwepo ongezeko kubwa la ajaili za barabarani ambazo nyingi husababisha vifo, ulemavu wa viungo pamoja na hasara nyengine za mali, hivyo kuna haja ya kuchukuliwa hatua za makusudi katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo. Dk. Shein alimueleza IGP Sirro haja ya kuitafutia ufumbuzi changamoto ya makaazi inayolikabili Jeshi hilo la Polisi kwa askari wake waliopo Zanzibar ili kuondokana na hali ya askari kuishi uraiani. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi zake za dhati kwa Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Nae Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania (IGP) Simon Sirro alitoa shukurani kwa Dk.Shein na kupongeza kwa mashirikiano makubwa inayoyapata Jeshi hilo kutoka kwa wananchi na viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha, IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuendeleza amani na utulivu walionao na kusisitiza haja ya kudumishwa na kuimarishwa zaidi kwa maslahi ya nchi na wananchi wake. Pia, Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi alimuhakikishia Dk. Shein kuwa hatua za makusudi zitachukuliwa katika kuhakikisha changamoto zilizopo kwa Jeshi la Polisi hapa Zanzibar zinapatiwa ufumbuzi sambamba na kuahidi kusimamiwa vyema suala zima la usalama wa barabarani. IGP Sirro aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli Mei 28, 2017 na kuapishwa Mei 29, 2017 Ikulu mjini Dar-es-Salaam. IGP Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambapo kabla ya kuteuliwa kushika cheo hicho alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Da-es-Salaam,ambapo pia, ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambaye ni Kamanda wa tatu wa Kanda Maalum ya Dar-es-Salaam.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo