Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Balozi Seif akutana na Ujumbe wa Viongozi wa Manispaa ya Potsdam kutoka nchini Ujerumani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba ipo haja kwa Miji ya Zanzibar na ule wa Potsdam wa Nchini Shirikisho la Ujerumani kubuni miradi ya pamoja inayofanana Kiuchumi ili isaidie kunufaisha Wananchi wa Miji hiyo Miwili. Alisema hatua hiyo itaendeleza ushirikiano wa Uhusiano wa muda mrefu uliopo baina ya Nchi za Miji hiyo inayofanana Kisiasa na Kimazingira kutokana ya Ujerumani Magharibi na Mashariki Kuungana pamoja na kuwa Taifa Moja Shirikisho kama zilivyo kwa Tanganyika na Zanzibar ziliyounda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Manispaa ya Potsdam iliyopo Mkoa wa Brandenburg Nchini Shirikisho la Ujerumani ukiongozwa na Meya wa Mji huo Bwana Jann Jackobs aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Alisema faida ya ushirikiano baina ya Miji ya Zanzibar na Potsdam kwa kipindi kirefu imeanza kuleta matumaini hasa ikizingatiwa ile miradi iliyoanzishwa kwa pamoja baina ya pande hizo mbili ya Nyumba za Maendeleo za Kikwajuni { Majumba ya Mjerumani } pamoja na uimarishaji wa Miundombinu ya Ujenzi wa Mitaro ya Maji Machafu katika Manispaa ya Zanzibar. Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake itazingatia na kuona namna gani inaweza kusaidia nguvu katika uratibu wa uendelezaji wa ushirikiano wa utendaji wa kila siku wa Miradi ya pamoja itakayoanzishwa na Miji hiyo miwili. Amehimiza umuhimu wa kuendeleaza mabadilishano ya ziara za mara kwa mara kati ya Viongozi, Watendaji na hata Wananchi wa kawaida wa Miji hiyo ikilenga kudumisha ushirikiano wa Kihistoria uliopo baina ya Ujerumani na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi huo wa Manispaa ya Potsdam unaoongozwa na Bwana Jann Jackobs kuwa Mbaalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar Kiuwekezaji Nchini Shirikisho la Ujerumani. Alisema Zanzibar hivi sasa iko mbioni kuendelea kuimarisha miundombinu katika sekta ya Utalii inayotegemewa kuwa muhimili mkuu wa Uchumi wa Taifa fursa ambayo wawekezaji wa Ujerumani wanaweza kuitumia katika kuweka vitega uchumi vyao katika sekta hiyo. Balozi Seif alisema Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea Zao la Karafuu ambalo limepitia katika mitihani mbali mbali katika vipindi tofauti kiasi kwamba mabadiliko ya soko la Dunia limeiwezesha Zanzibar wakati mwengine kusua sua katika ushumi wake. Mapema Meya wa Manispaa ya Potsdam Bwana Jann Jackobs alisema mambo ya msingi ya ushirikiano kati ya Mji wa Potsdam na ule wa Zanzibar yameshakubalika na tayari yanawekwa saini kipindi hichi kwa ajili ya utekelezaji wa pamoja. Bwana Jackobs alielezea faraja yake kutokana na sekta ya Utamaduni na Utalii kuanza kuonyesha matumaini ya mafanikio hasa katika baadhi ya matamasha yanayofanyika moja kati ya pande hizo kushirikisha wadau wa sehemu zote mbili. Hata hivyo Meya wa Manispaa hiyo ya Potsdan alifafanua wazi kwamba masuala ya mazingira na fursa za ajira hasa kwa Vijana yanakusudiwa kufanyiwa utaratibu wa utekelezaji wake katika kipindi kifupi kijacho ili kuja kusaidia kustawisha maisha ya Vijana wengi. Manispaa ya Potsdam iliyomo ndani ya Mkoa wa Brandenburg Kilomita 15 Kusini Magharibi mwa Mji wa Berlin Nchini Shirikisho la Ujerumani ina wakaazi wapatao Laki 167,745 kwa mujibu wa sensa ya Watu ya Mwaka 2015 ikilinganishwa na Manispaa ya Mji wa Zanzibar yenye wakaazi Laki 223,000 kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2012.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo