Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Awatunuku Wahitimu wa Chuo Cha Taifa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mafunzo makini yanayozingatia nidhamu na uadilifu katika kuwapatia mafunzo ya Uongozi Watendaji wa Serikali na Taasisi mbali mbali za Umma ndio kigezo pekee kitakachoendelea kulinda heshima ya Taifa kwa kuzingatia misingi ya amani na utulivu. Balozi Seif alitoa kauli hiyo wakati akiyafunga mafunzo ya Stashahada na Shahada kwa wanafunzi wa mkupuo wa Tano wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania { NDC } yaliyofanyika katika Kampas ya chuo hicho kiliopo Kunduchi Jijini Dar es salaam. Alisema uwajibikaji uliotukuka ambao hupatikana ndani ya Taasisi za Umma huongezeka pale Viongozi husika wanaopata mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa dhama wanazokabidhiwa na Umma. Balozi Seif alisema yapo mabadiliko makubwa ya kiutendaji yaliyokwishapatikana ndani ya Taasisi mbali mbali za Umma ambazo Viongozi wake wameshapata mafunzo ya kuwajengea uwezo tokea kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Nchini. Alifahamisha kwamba Serikali zote mbili iloe ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kukiunga mkono Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania {NDC}katika azma yake ya kuwafinyanga Viongozi na watendaji wa Taasisi za Umma kuwa na utumishi uliotukuka. Akizungumzia suala la amani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliviagiza vyombo vya Ulinzi Nchini kuendelea kulinda mipaka, mali na usalama wa Wananchi ili Tanzania iendelee kubakia kuwa kisiwa cha Amani Duniani. Balozi Seif alisema amani iliyopo Nchini hivi sasa ambayo hata baadhi ya Wananchi wa Mataifa jirani wanaitumia kwa kutafuta usalama wao kutokana na migogoro wanayoikimbia inafaa kulindwa na kuenziwa kwa nguvu zote. Alisema Serikali zote mbili hazitakuwa na mjadala na kikundi au Mtu yeyoyete katika kuzingatia usalama wa Taifa ambao juhudi zitachukuliwa wakati wote katika kuhakikisha maisha ya wananchi na raia zake wanaendelea na harakati zao za kimaisha bila ya bughudha yoyote. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi mzima wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania kwa jitihada unazochukuwa na hatimae kupelekea wanafunzi kutoka Mataifa mbali mbali Duniani kuhamasika na kuamua kujiunga na Chuo hicho. Mapema Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania Meja General Yaqoub Hassan Mohamed alisema Chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya Stashahada na Shahada kwa wanafunzi mbali mbali ndani na nje ya Nchi tokea kuanzishwa kwake miaka Mitano ilitopita. Kamanda Yaqoub alisema mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yamejikita katika usalama na Mikakati pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Usalama na Mikakati nayayokwenda sambamba na mafunzo ya muda mfupi katika kuwajengea uwezo Makatibu Wakuu , Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Taasisi za Umma. Mapema Katibu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania Brigedia General Mabongo alisema jumla ya wahitimu 10 wa Stashahada ya Usalama na Stratejia wamefanikiwa kutunukiwa tuzo katika Mkupuo huo wa Tano baada ya kufaulu vyema kwenye mafunzo yao. Brigedia General Mabongo alisema kwa upande wa Shahada ya Uzamili ya Usalama na Stratejia jumla ya wahitimu 35 wamehitimu mafunzo yao miongoni mwao wakapatikana wanafunzi bora waliotunukiwa medani kutokana na umahiri wao. Alisema wanafunzi hao mchanganyiko na makamanda wa Vikosi tofauti vya Ulinzi wametoka katika Mataifa mbali mbali duniani ikiwemo Rwanda, Afrika Kusini,Zamziba, Zimbabwe, Nigeria, Burundi, Malawi, Kenya, Namibia, Botswana, China na wenyeji Tanzania.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo