Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
China National Research Institute of Food Fermentation Industries imezinduliwa na Mhe.Gavu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Issa Haji Gavu amezindua mafunzo ya mapishi na ukarimu yatakayoendeshwa na Taasisi ya ‘China National Research Institute of Food Fermentation Industries’ kutoka nchini humo na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa msaada wao huo wa mafunzo. Mafunzo hayo yaliyoanza leo 18 Septemba hadi 29 Septemba mwaka huu ni kwa ajili ya watendaji wa Serikali wanaotoa huduma za upishi na ukarimu kwa viongozi wakuu wa nchi pamoja na walimu kutoka Taasisi ya Utalii iliyopo Maruhubi. Hafla hiyo ya ufunguzi ilifanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni mjini Zanzibar, na kuhudhuriwa na vionghozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi mdogo wa China Xie Xiaowu na Makamo wa Rais wa Taasisi ya China National Research Institute of Food Fermentation Industries. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Waziri Gavu aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kukubali ombi la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapnduzi Dk. Ali Mohamed Shein la kutoa mafunzo kwa watendaji hao wa Serikali. Alisema kuwa uamuzi wa maunzo kufanyika hapa Zanzibar unatoa uhueni na nafuu ya gharama za uendeshaji na utoaji nafasi kubwa zaidi kwa watendaji wanapata mafunzo hayo kufahamu mambo mambo watakayofundishwa katika mazingira ya nyumbani waliyoyazoea na wanyoyafanyia kazi. Waziri Gavu alitoa pongezi kwa timu kabambe ya viongozi, wakufunzi na wasimamizi kutoka taasisi hiyo imekuja Zanzibar kwa jaili ya kufanikisha mafunzo hayo huku akitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kukubali kuendesha mafunzo hayo katika Taasisi ya Utalii iliyopo Maruhubi. Aidha, aliwataka wakufunzi hao kuitumia fursa hiyo kwa kuitembelea na kuifahamu historia ya Zanzibar,kufurahia mazingira yake pamoja na ukarimu wa watu wake na kueleza kuwa licha ya kuwa muda ni mdogo wameandaliwa safari ya matembezi katika Kisiwa cha Pemba ili waweze kupata fursa ya kuona na kufurahia mazingira. Waziri Gavu alitoa pongezi kwa Balozi mdogo wa China Xie Xiaowu kwa juhudi zake alizozichukua hadi kuhakikisha kuwa dhamira ya kutoa mafunzo hayo inafanikiwa na inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Sambamba na hayo, Waziri Gavu alieleza kuwa mafunzo hayo yana umhimu mkubwa kwa watendaji hao na kwa nchi nzima kwa jumla kwa vile wao wanajukumu la kuhudumia viongozi wa nchi pamoja na wageni mashuhuri wanaofika nchini. Pia aliwaeleza watendaji hao kuwa umri wao wengi bado unaonesha kwua wanayo nafasi kubwa ya kujiendeleza kimasomo na kusisitiza kuwa eneo la taaluma lina umhimu mkubwa katika Serikali na jamii nzima kwa jumla. Mapema Balozi Mdogo wa China anaefanya kazi zake Zanzibar Xie Xiaowu alisema kuwa mafunzo hayo ni ya kwanza kufanyika hapa Zanzibar ambayo yatawajumuisha watendaji 30 kutoka taasisi za Serikali. Alisema kuwa tokea mwaka 2005 Taasisi hiyo imeshatoa mafunzo 82 kwa watendaji kwa nchi zinazoendelea kutokana na msaada wa Serikali ya China hatua ambayo imezidisha uhusiano na ushirikiano kwa nchi hizo. Aliongeza kuwa mafunzo hayo si muhimu tu kwa upande wa maendeleo ya Zanzibar bali inatoa picha kwa Zanzibar katika kuendeleza soko la ajira sambamba na juhudi za kupambana na umasikini na kusisitiza kuwa mafunzo hayo ni mazuri wka Zanzibar na itaipelekea Zanzibar kuimarika kiuchumi na kijamii. Nae Makamo wa Rais wa Taasisi ya ‘China National Research Institute of Food Fermentation Industries’ kutoka nchini China Hung Yutong alitoa pongezi kwa viongozi waliobuni mafunzo hayo ambayo yana umuhimu mkubwa kwa watendaji wa Serikali katika kuiendeleza nchi na watu wake. Kiongozi huyo alieleza kuwa Zanzibar ni nchi nzuri yenye mazingira yaliofanana na nchi ya Switzeland ambayo ina vivutio vingi vya kitalii ukiwemo Mji Mkongwe wake ambao ni urithi wa Kimataifa kama ulivyochanguliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO. Hung Yutoung alieleza jinsi wakufunzi walivyojipanga kutoa mafunzo hayo ambayo yatawawasaidia kwa kiasi kikubwa watendaji hao. Sambamba na hayo, Yutong alieleza kuwa mafunzo hayo yatakuwa ni daraja katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano pamoja na kuweza kubadilishana utaalamu katika mapishi ya vyakula hatua ambayo pia, itaimarisha ushirikiano katika sekta ya utalii.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo