Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Hafla ya utiaji saini ujenzi wa Barabara nne za Unguja
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo imetiliana saini Mkataba wa Ujenzi wa Bara Nne za Bububu- Mahonda- Mkokotoni, Pale Kiongele, Matemwe – Muyuni na Fujoni – Kombeni zinazotarajiwa kuwa na urefu wa Kilomita 52. Mkataba huo uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A” uliopo Mkokotoni ulishuhudiwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali na Kisiasa wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Saini ilitiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Nd. Mustafa Aboud Jumbe wakati ule wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi ya China { CCECC } inayojenga Bara bara hizo ulitiwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Nchini Tanzania Bwana Jiang Yi Giao. Ujenzi wa Mradi huo wa Bara bara ambao ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 -2020 unagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mkopo nafuu wa fedha wa Shilingi Bilioni 58 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika { ADB }. Akizungumza mara baada ya utiaji saini Mkataba huo wa Ujenzi wa Bara bara Nne za Unguja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar isingependa kuona inaingia katika migogoro na Wajenzi wa Miradi tofauti. Balozi Seif alisema zipo Kampuni zilizowahi kutiliana saini Mikataba ya Ujenzi wa Miundombinu ya Bara bara na hatimae Kampuni hizo zikaingia mitini na kushindwa kukamilisha Mikataba ya Miradi waliyoikubali. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Wananchi watakaohusika na maeneo yatakayopita Miradi hiyo ya Bara bara wasaidie kuharakisha Miradi hiyo ili imalizike kwa wakati uliopangwa. Alisema changamoto za ulipaji wa fidia za Majengo pamoja na vipando vya Wananchi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Mradi huo isiwe vikwazo vya kuviza mpango wa Maendeleo uliokusudiwa kufanywa na Taifa. Mapema Kaimu Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alisema Mradi huo wa Bara bara utahudumia watu wote bila ya ubaguzi au itikadi za Kisiasa. Hivyo Mh. Ayoub alionya kwamba Mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuzuia kuendelea kwa miradi hiyo Serikali haitosita kumchukuliua hatua zinazofaa za kinidhamu. Alisema ni vyema kwa Wananchi wawe tayari kuipokea miradi hiyo sambamba na kushirikiana na Serikali pamoja na Wajenzi wa Mradi huo ili kuhakikisha inafanikiwa na kuleta tija kwa Jamii yote Nchini. Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Balozi Ali Karume alisema kuimarika kwa Miundombinu ya Bara bara Nchini ni chachu ya Maendeleo kwa Taifa. Balozi Karume alisema usumbufu wa usafiri kwa Wananchi wanaoishi katika maeneo utakayopita Mradi huo unatarajiwa kuwa Historia baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Bara bara hizo. Waziri wa Ujenzi, Miundombinu na Usafirishaji aliwaomba Wajenzi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi ya China { CCECC } kuhakikisha kwamba mradi huo unakamilika kwa wakati uliomo kwenye Mkataba wa Ujenzi. Akitoa salamu za Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi ya China { CCECC } Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tawi la Tanzania Bwana Jiang Yi Giao aliihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Utaalamu na uzoefu iliyonayo Kampuni hiyo ndio shahada inayothibitsha wazi kwamba kazi za Taasisi hiyo zinafanywa kwa sheria na Taratibu zilizopo. Bwana Jiang alisema Kampuni ya CCECC iliyoasisiwa mnamo mwaka 1979 tayari ina uzoefu mkubwa uliopelekea kuwa miongoni mwa Makampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi 100 yaliyopo Duniani. Alisema Kapuni hiyo ya ujenzi imeshakuwa maarufu Duniani likiwemo Bara la Afrika ambapo Miradi mbali mbali imeshajenga ikiwemo Reli ya Tanzania na Zambia, Bara bara na Madaraja ya kisasa katika Miji mingi Barani Afrika yakiwemo Majengo makubwa ya huduma za Jamii pamoja na Kijiji cha Kisasa Nchini Rwanda. Bwana Jiang alifafanua kwamba CCECC pia imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia miradi ya Kijamii kwa Wananchi wa Mataifa yanayofunga Mikataba ya Ujenzi wa Miradi tofauti ya Maendeleo na Kampuni hiyo. Bara bara ya Bububu –Mahonda – Mkokotoni itajengwa na kupanuliwa upana wa Mita 8 wakati nyengine Tatu zilizobakia zitajengwa kwa upana wa Mita 6 chini ya usimamizi wa Taasisi ya Gauff kutoka Nchini Ujerumani.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo