Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za Polisi kisiwani Pemba, wadau wachangia milioni 400
NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini na kufanikisha kupata vifaa vya ujenzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa nyumba za Polisi Mikoa ya Pemba, Zanzibar. Mradi huo umeanza katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo nyumba kumi na mbili zinatarajiwa kujengwa ili kufanikisha askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi ndani ya mikoa hiyo waweze kuishi katika nyumba za jeshi pamoja na kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za makazi ya polisi hao, pia mradi huo utajenga nyumba katika mikoa mipya nchini pamoja na makao ya nchi Dodoma. Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, katika Bandari ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, jana, Mhandisi Masauni alisema, ujenzi wa nyumba hizo utakua ni wa hatua ya awali, lakini mipango mbalimbali itaendelea kuwezesha nyumba nyingi zaidi kujengwa katika eneo hilo ili kuhakikisha baadhi ya askari wanaoishi nje ya kambi za polisi waweze kuishi kambini ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi. “Leo nimewakabidhi wakuu wa mikoa hawa vifaa vya ujenzi ambavyo ni mifuko ya saruji, nondo, ndoo za rangi na mabati ili waweze kusimamia zoezi hili la ujenzi wa nyumba za askari wetu kwa umakini mkubwa,” alisema Masauni na kuongeza; “Tunajenga nyumba hapa Pemba ni mradi wa awamu ya kwanza, kwa awamu ya pili tutaenda katika maeneo mengine ya nchi, hususani mikoa mipya yaSimiyu, Geita, Katavi na Songwe na pamoja na Makao ya nchi Dodoma, kwa kuwa askari wetu hawa wanafanya kazi kubwa sana kwa kuwalinda raia wa nchi hii kuendelea kuwa salama kwa wao wenyewe pamoja na mali zao.” Alisema anawashukuru wadau mbalimbali kwa kujitolea kutoa vifaa hivyo ili kufanikisha suala hilo na aliwataka watanzania wawe na moyo kama wadau hao kwa kuipenda nchi yao, kupenda maendeleo kwa kutoa misaada mbalimbali. Masauni alifafanua kuwa, suala la maendeleo halina siasa, tuijenga nchi, katika mazingira mengi ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa maana ya Unguja katika suala la kujitolea wamekua wanafanya hivyo, ila kuna changamoto kidogo kwa upande waPemba pana tatizo la masuala ya kisiasa, watu wamekua wakiingiza siasa mbele katika masuala ya nchi katika mikoa hiyo ya Pemba, ambapo alisema jambo hilo sio jema katika maeneleo ya nchi. “Serikali zote mbili ya Bara na Visiwani zipo kuwahudumia wananchi wote, wakati wa siasa umepita, sasa hivi tunataka kila mmoja ashiriki katika masuala yote ya kimaendeleo, askari hawa wanaangalia usalama wa watu wote, bila kujali hitikadi, dini ya mtu, wapi anatoka, bila kujali rangi yake bila kujali kabila lake,” alisema Masauni. Alisema viongozi wa Serikali katika mikoa ya pemba wamekua wakipata tabu kuhamasisha katika masuala mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao, hivyo wao kama serikali kuu wameamua kupeleka maendeleo katika maeneo ambayo yanakua yana tabu katika kuhamasisha masuala ya maendeleo, hivyo wakaamua waje mikoa hiyo ya Pemba katika awamu hiyo ya kwanza ya mradi. Akizungumzia ujio huo wa Naibu Waziri pamoja na ujenzi wa nyumba hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, alisema anamshukuru kiongozi huyo kwa kuwaletea maendeleo hayo makubwa ya ujenzi wa nyumba za polisina kumuhkikishia vifaa walivyopokea watasimamia ujenzi wa nyumba hizo kwa nguvu zao zote. “Sisi wakuu wa mikoa tunakushuru naibu waziri kwa hili ulilolifanya, tunakuhakikishia tutasimamia ujenzi huu kwa juhudi zote mpaka nyumba zitakapokamilika, tunasema asante sana kwa kuhamasisha wadau na hatimaye kufanikiwa kupata vifaa hivi,” alisema Mwajuma.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo