Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
SMZ yaving’arisha vijiji vya Mlilile, Mbuyumaji kwa umeme
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, amesema mapinduzi ya Zanzibar ndio yaliyowakomboa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba kutoka kwenye makucha ya ukoloni. Akizungumza katika ufunguzi wa mradi wa kupeleka umeme katika kijiji cha Mlilile Matemwe Wilaya ya Kaskazini A ikiwa miongoni mwa shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi. Waziri huyo alisema si vyema kuyapuuza Mapinduzi hayo, akisisitiza wale wanaoyabeza wasipewe nafasi kwani huenda wana ajenda ya siri. Aidha, aliwataka wananchi wa Unguja na Pemba kuyaenzi matunda ya Mapinduzi hayo ambayo lengo lake ni kuwainua wananchi wanyonge kwa kuwaletea maendeleo yatakayoinua ustawi wa maisha yao na kuwafanya watembee kifua mbele. Waziri Haroun alifahamisha kuwa, iko haja kwa wananchi kushirikiana kwa pamoja katika kuijenga nchi, kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haimbagui mtu kwa sura yake au eneo analotoka. Hata hivyo aliwaomba wananchi wa kijiji cha Mlilile kutumia fursa waliyoipata kwa kutumia huduma ya umeme katika kazi za ujasiriamali pamoja na miradi mingine itakayoweza kuwaingizia kipato. Akitoa taarifa ya kitaalamu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk, alisema serikali imelipa jukumu shirika lake kusambaza huduma ya umeme kwa wananchi hadi katikia maeneo yao popote walipo. Alisema kazi ya usambazaji umeme vijijini itaendelea kufanywa na serikali hatua kwa hatua ili kuwawezesha wananchi wote kunufaika na huduma hiyo. Alieleza kuwa, mradi huo katika kijiji cha Mlilile umegharimu shilingi 70,128,721.00 fedha zilizotolewa na Serikali kupitia ZECO. Alisema utekelezaji wa mradi huo, umefanywa kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika Mkoa wa Kaskazini mwezi Septemba 2017. “Katika ziara hiyo, Dk. Shein alitoa agizo la kufikisha umeme kijijini hapa ndani ya kipindi cha miezi sita, lakini ZECO imekamilisha kazi hiyo kwa miezi mitatu tu,” alieleza Mbarouk. Mradi mwengine kama huo, pia umezinduliwa katika kijiji cha Mbuyumaji Wilaya ya Kaskazini A na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Khalid Salum Mohammed, ambao umegharimu shilingi 79,000,000, ikiwa miongoni mwa shamrashamra hizo za Mapinduzi.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo