Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Ardhi yote ya Zanzibar ni mali ya Serikali
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar tangu baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ardhi yote ya Zanzibar ni mali ya Serikali na kuwashangaa wale wanaoiubuka na kudai ardhi kuwa ni zao na kuanza kuziuza.Rais Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mji wa Kisasa huko Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, mji ambao uko katika Maeneo huru ya Kiuchumi. Alieleza kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ataitunza ardhi ya Zanzibar kwa manufaa ya watu wa Zanzibar na yeye Rais atamteua Waziri na ampe dhamana ya kusimamia ardhi hiyo, na kueleza kuwa mwananchi anapewa hati ya kutumia ardhi na sio hati ya kumiliki ardhi kwani hakuna nchi duniani inayouza ardhi yake ama kukodisha bila ya kufuata taratibu zilizopo.Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Serikali ndio yenye mamlaka ya kuhaulisha matumizi ya ardhi kwa malengo mbali mbali na iwapo Serikali itahitaji kuitumia ardhi inalazimika kutoa fidia za mali za wananchi zilizopo kwenye eneo hilo kama vile nyumba na vipando vya miti vya kudumu. Dk. Shein alisema kuwa ujenzi wa miji ya kisasa na nyumba za maendeleo ni fikra ya Kimapinduzi ya kujenga nyumba zilizo bora, zinazozingatia mahitaji muhimu ya familia pamoja na kuzijenga kwa mpangilio maalum.Alisema kuwa wananchi walio wengi walikuwa wakiishi katika nyumba duni, nyingi zao zikiwa zimetengenezwa kwa miti na udongo na kuezekwa kwa makuti au madebe ambapo mara baada ya Mapinduzi, Serikali iliamua kuanza kutekeleza ahadi za Chama cha ASP za kuwawekea makaazi bora ya kisasa wananchi wote wanyonge. Alisema kuwa hatua nyengine ya ujenzi wa nyumba za maendeleo ni ujenzi wa nyumba za Michenzani, Kikwajuni, Kilimani pamoja na sehemu nyengine mbali mbali za mjini na vijijini Unguja na Pemba ambapo kwa upande wa Pemba nyumba za maendeleo zilijengwa Wete, Machomane, Madungu Chake Chake, Micheweni, Kengeja na Mkoani.Dk. Shein alisema kuwa Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 yana neema kubwa sana ikiwa ni pamoja na kuwakomboa wanyonge ikiwa ni pamoja na kuwapa wanyonge hao nyumba bora kama alivyofanya Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Alisisitiza kuwa dhamira ya kuendeleza ujenzi wa miji ya kisasa imeendelezwa na uongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Awamu ya Saba kwa kushirikiana na wawekezaji na kuwapongeza wawekezaji kwa kushirikiana na Serikali na kuanzisha mradi huo hapa Zanzibar.Alisema kuwa mradi huo hauko katika nchi za Afrika na uko Zanzibar pekee ambao ni nyumba za kisasa huku akimpongeza Dk. Salmin Amour Juma kwa kuliweka eneo la Fumba na Micheweni kuwa Maeneo Huru ya Kiuchumi ambapo leo Fumba imefumbuka. Alisema kuwa yale yaliyofanywa Dubai ndio yatakayofanywa hapa Zanzibar kwani wawekezaji wameamua kuja kuekeza Zanzibar kutokana na maendeleo yaliopo sambamba na amani na utulivu. Nae Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Khalid Salum Mohamed alieleza kuwa mradi huo unatekelezwa ni katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 katika Ibara yake inayotaja maeneo ya Fumba na Micheweni na kumpongeza Dk. Shein kwa kusimamia vyema Ilani hiyo.Aliendelea kutoa pongezi kwa mwekezaji huku akiahidi kuwa juhudi kubwa zinafanywa ili kuhakikisha na Maeneo Huru ya Micheweni nayo yanaimarika kama ilivyo kwa Fumba huku akiipongeza Mamlaka ya Kukuza Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA). Dk. Khalid alisema kuwa katika uongozi wa Dk. Shein uwekezaji umeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo mnamo mwaka 2016 kulitekelezwa miradi 18 na mwaka 2017 miradi 42 ambapo tokea mwaka 2014 hadi 2017 jumla ya miradi 123 yenye gharama ya Dola Bilioni 1.5.Pia, alisema jumla ya ajira 5485 zimepatikana sambamba na kuimarika kwa huduma za kijamii na kuimarika kwa uwekezaji, kuimarika kwa mzunguko wa fedha sambamba na kuongeza mapato kwa serikali huku akiwaahidi wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kuweka Sera na Sheria nzuri katika kuwavutia wawekezaji. Aliongeza kuwa juhudi za makusudi zinachukuliwa katika kuhakikisha suala la makaazi linaimarika kwa kasi na kuweza kukuza uchumi kama ilivyoimarika kwa nchi nyingi duniani na kueleza kuwa miji mengine 14 midogo itajengwa hapa Zanzibar. Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar alisema kuwa eneo la Fumba lenye Hekta 3000 lilitangazwa rasmi kuwa Maeneo Huru ya Kiuchumi mnamo mwaka 1992 sambamba na eneo la hekta 808 lililopo Micheweni Pemba.Alieleza kuwa Mradi wa Mji wa Fumba unaotekelezwa na Kampuni ya CPS Live Company Ltd ni mojawapo wa miradi mikubwa iliyoidhinishwa na Mamlaka ya Kukuza Vitega Uchumi (ZIPA) kuwekeza katika maeneo Huru ya Kiuchumi ya Fumba.Alieleza kuwa Mradi huo unamilikiwa na Raia watatu wa Ujerumani na mmoja wa Ubelgiji ambapo kwa upande wa Raia wa Ujerumani ni Bwana Sebastian Dietsold anayemiliki kwa asilimia 40, Bi Katrin Dietsold asilimia 40 na Bwana Tobias Dietsold asilimia 18 na asilimia 2 zilizobaki ndio zinamilikiwa na Raia wa Ubelgiji Johan Aberebe. Mradi unatarajiwa kuwekeza jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 250 kwa awamu nne ambapo utakuwa na nyumba 1400 ambapo zitajengwa katika mfumo wa nyumba za chini, nyumba za roshani moja hadi sita ambapo utekelezaji wake utakuwa katika awamu 4 ambapo bei ya kuanzia kwa nyumba itakuwa TZS 37 milioni.Alisema kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo inakusudia kujenga nyumba 720, nyumba za kawaida 237 na mbele ya bahari nyumba 34 na hivyo kufanya jumla ya nyumba zinazojengwa katika awamu hiyo zinatarajiwa kukamilika katika mwishoni mwa mwaka 2019 kufikia nyumba 991 ambapo nyumba 60 zinatarajiwa kukabidhiwa wanunuzi mwezi Juni mwaka huu. Mradi huo unatumia teknolojia ya ujenzi inayotumia rasilimali kidogo ya mchanga bila ya kuathiri ubora wa nyumba hizo na kwa kuzingatia mahitaji maalum ya nchi kama Zanzibar yenye joto na vipindi vya mvua ambapo mradi umewekeza katika kiwanda cha kujenga kuta maalum za nyumba za mbao na tayari kiwanda kinafanya kazi hiyo. Nae Sebastian Dietsold ambaye ndie mkuu wa mradi huo alieleza hatua zilizofikiwa katika Mradi huo na kuahidi kuwa mradi huo utaendelea kuwa wa aina yake hapa Zanzibar na kueleza jinsi walivyokusudia mradi huo kuwasaidia na wananchi wenye kipato cha chini.Alieleza changamoto waliyonayo ya barabara hadi kufikia katika mradi wao huo na kutoa ombi la kujengewa barabara hiyo ambapo Waziri wa Fedha Dk. Khalid Mohamed alimuahidi kuwa Serikali italifanyia kazi ombi lake hilo na kuijenga barabara hiyo. Aidha, alieleza kuwa tayari kuna mashirikiano mazuri kati ya Kampuni hiyo na Benki ya PBZ na kueleza haja kwa wananchi kutumia fursa hiyo kukopa fedha kwa ajili ya kununua nyumba ambazo zinajengwa na kampuni hiyo.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo