Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Balozi Seif: Serikali haitomuonea huruma mtu yeyote akijenga sehemu bila ruhusa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya na kusisitiza kwamba Serikali haitomuonea huruma Mtu ye yote atakayeamua kujenga Nyumba au jengo lolote katika eneo lisilopata ridhaa ya Taasisi inayohusika na masuala ya Ujenzi, Ardhi, Mipango Miji na Vijiji. Alisema hivi sasa ipo tabia ya muhali inayoonekana kuendelea kufanywa na baadhi ya Viongozi wanaopewa jukumu la kusimamia Sheria na Taratibu za Serikali kiasi kwamba watu huamua kuchukuwa sheria mikononi mwao. Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua eneo ambalo Serikali kuu inatarajia kujenga Hospitali Kubwa ya Rufaa katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja. Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshaamua kudhibiti wimbi la ujenzi holela katika maeneo mbali mbali hasa yale yaliyotengwa kwa ajili ya Kilimo na Miradi mengine ya Maendeleo. Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kuhakikisha kwamba eneo hilo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Hospitali linakuwa katika udhibiti unaostahiki. Akitoa maelezo ya eneo hilo Mkurugenzi Idara ya Tiba Dr. Mohamed Dahoma alisema eneo hilo lenye ukubwa wa Hekta 83 hivi sasa liko kwenye udhibiti wa Wizara ya Afya kwa ajili ya mpango wa baadae wa Ujenzi wa Hospitali Kubwa ya Rufaa. Dr. Dahoma alimueleza Balozi Seif kwamba Wizara ya Afya kupitia wataalamu wa uchambuzi yakinifu inaendelea na uhakiki wa eneo hilo kwa lengo la kufanya michoro itakayotoa muelekeo mzima wa uendelezaji wa mradi huo utakavyokuwa. Alisema Mradi huo mkubwa utakaokwenda kwa Awamu Tatu umepangwa kuwa na Kitengo cha Mafunzo, Hospitali ya kulazwa Wagonjwa baina ya Mia Mbili na Mia Tatu, Nyumba za Wafanyakazi pamoja na Majengo ya Utawala. Mkurugenzi Tiba wa Wizara ya Afya alifafanua kwamba Majengo yaliyokuwemo ndani ya Eneo hilo hapo awali yalikuwa ya Taasisi ya African Muslim Agency kwa ajili ya ujenzi wa Skuli lakini Serikali iliamua kulichukuwa eneo hilo kwa ajili ya Mradi mkubwa zaidi wa Kijamii Nchini. Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitembelea Majengo ya kitakachokuwa Chuo cha Marekebisho ya Watu walioathirika na Dawa ya Kulevya { Sober House } liliopo katika Kiji cha Kidimni Wilaya ya Kati. Mshauri Muelekezi wa Mradi huo Nd. Mbwana Bakar Juma alimueleza Balozi Seif kwamba mradi huo tayari umeshakamilika katika Awamu ya kwanza kwa uwepo wa Ofisi, Jiko pamoja na Bweni la kulala Waathirika hao. Bwana Bakar alisema Mkandarasi wa Ujenzi huo Kampuni ya Kizalendo ya Al – Hilal General Traders licha ya mradi huo tayari kuukabidhi Serikalini lakini hivi sasa Wahandisi wake wanaendelea kufanya uhakiki wa maeneo ambayo yana hitilafu yoyote ili kuyafanyia marekebisho. Mshauri Muelekezi huyo alifahamisha kwamba Majengo hayo yatakapokamilika kabisa yatakuwa na sehemu za Kilimo, Karakana ya Mafunzo ya Ujasiri amali, Wafanyakazi pamoja na eneo la michezo kwa Vijana watakaokuwa wakiishi sehemu hiyo. Naye Mkurugenzi Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bibi Halima Ramadhan Toufiq alisema Mradi huo hadi hivi sasa tayari umeshagharimu Jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni Mia 6.9 katika hatua ya Awamu ya Kwanza. Bibi Halima alisema awamu ya Pili unaotarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Bilioni Nne za Kitanzania utaongezwa ghorofa katika Ofisi ya Utawala na Majengo mengine pamoja na kutengenezwa miundombinu ya Maeneo ya kilimo na viwanja vya Michezo.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo