Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa ZBC Wakati wa Ziara Yake Katika Majengo ya ZBC Redio Rahaleo Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewashauri Wana Habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC} kuendelea kuwa wabunifu zaidi wa vipindi vitakavyoleta mvuto na hatimae kuwa na wasikilizaji wengi zaidi wa Shirika hilo Nchini. Alisema licha ya kuwepo kwa vipindi vingi vilivyokuwa maarufu na kukubalika kwa wasikiizaji wengi akitolea mfano Kipindi cha Mawio na Maelezo baada ya Habari lakini bado juhudi za ubunifu zinahitajika katika kuona Mfumo wa Matangazo unawafikia Wananchi wengi zaidi Mjini na Vijijini. Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati alipofanya ziara fupi katika Kituo cha Matangazo cha Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC – REDIO} kiliopo Rahaleo Mjini Zanzibar kuangalia shughuli za utendaji kazi wa Taasisi hiyo ya Habari na kuridhika na jitihada zinazochukuliwa na Watendaji wawake. Alisema upo umuhimu wa vipindi na matangazo ya ZBC Redio kuangaza zaidi kwa upande wa Majimboni na Vijijini ili Wananchi wa maeneo hayo wawe na fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili hasa katika harakazi zao za kujiletea maendeleo. Balozi Seif alieleza kwamba wakati Serikali Kuu inafikiria jitihada za kusaidia changamoto zinazowakabili watendaji wa Kituo hicho cha Matangazo ya Radio ambapo pia kupitia nafasi yake ya Uwakilishi atajaribu kuwashawishi Wawakilishi wenzake majimboni kutoa ushirikiano utakaowezesha kuendelezwa kwa Vipindi vya kutoka Majimboni. Alisema vipo vipindi vinavyoweza kusaidia Wananchi kuelimika zaidi ambavyo vinapaswa kupewa umuhimu wa pekee ili kupunguza kero zinazowakabili sambamba na kumrahisishia Mwakilishi kutekeleza majukumu yake badala ya kusubiri Vikao vya Baraza la Wawakilishi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliutaka Uongozi wa Shirika la Habari Zanzibar kupitia Wizara yake ya Habari, Utalii na Mambo ya kale kutoa kipaumbele masuala ya vitendea kazi vinavyohitajiwa na watendaji na kuainishwa ndani ya Bajeti ya Shirika badala ya kusubiri Serikali Kuu. Hata hivyo Balozi Seif alisema mpangilio wa maombi hayo ni vyema ukafanyika kwa kila Awamu kwa vile hakutakuwa na Bajeti itakayokuwa na uwezo wa kutosheleza mahitaji ya kila Taasisi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza utaratibu wa kuendeleza Vikao vya utendaji kati ya Uongozi wa Shirika na Wataendaji wake ili kutafuta njia ya kutanzua kasoro zinazojichomoza ndani ya uwajibikaji wa Wafanyakazi na Viongozi wa Taasisi hiyo. Alisema licha ya vikao hivyo kuibua mapungufu ya utendaji ndani ya kazi lakini pia vitasaidia kupunguza au kuondoa minong’ono ya umbali unaoweza kujitokeza kati ya pande hizo mbili. Balozi Seif alifahamisha kwamba mapenzi kati ya Viongozi na Wafanyakazi hao ni jambo la msingi na la muhimu hasa kutokana na muingiliano wa kazi zao kwa vile zinategemeana. Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitembelea vitengo mbali mbali vya Kituo hicho cha Matangazo ya Redio cha Shirika la Utangazaji Zanzibar na kujionea uwajibikaji wa Kizalendo waliokuwa nao watendaji wake ambao umempa faraja kubwa. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC} Bibi Iman Duwe alimueleza Balozi Seif kwamba Jengo la Kituo hicho linatarajiwa kufanyiwa matengenezo makubwa chini ya Usimamizi wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China. Bibi Iman alisema Matengenezo hayo yanayotarajiwa kuanza mara baada ya kukamilika Mradi ya Matengenezo uliopo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja utahusisha marekebisho ya Jengo sambamba na ufungaji wa vifaa vyengine vipya vinavyokwenda na mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano Ulimwenguni. “ Tunatarajia kupata Mitambo mengine Mipya ya Digital itakayoenda sambamba na Mafunzo ya Miezi sita kwa Watendaji wake”. Alisema Mkurugenzi Mkuu huyo wa Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC}. Balozi Seif aliangalia utendaji kazi ndani ya Chumba cha Habari, baadhi ya Studio za Vipindi na Kutangazia, Maktaba ya Vipindi vya Redio, pamoja na chumba maarufu cha kipindi cha Mawio.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo